Pre GE2025 Kasesela: Mbunge au Diwani atakayeshindwa kutetea nafasi yake ajilaumu mwenyewe

Pre GE2025 Kasesela: Mbunge au Diwani atakayeshindwa kutetea nafasi yake ajilaumu mwenyewe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wanajukwa!

Kwahiyo huyu Kasesela anataka kuwapa jeuri gani au anataka kuwapoteza wenzie?

Kila mtu atapita kwa kipimo cha kazi aliyoifanya kama alifanya uozo basi itakula kwake na awamu hii naona wengi watarudi makwao vichwa chini!
===================

Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa (MNEC) Richard Kasesela amesema kuwa Mbunge au Diwani atakayeshindwa kutetea nafasi yake ajilaumu mwenyewe kwa kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekeleza makubwa kwenye kila jimbo na kata kulingana na ilani ya CCM ya 2020/2025.

Kasesela aliyasema hayo katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa, ambapo alisisitiza kuwa kazi kubwa zilizofanywa na Rais Samia zinawapa urahisi viongozi waliopo kuendelea na nafasi zao na iwapo watashindwa, ni wao wenyewe watakaojilaumu.

Soma Pia: Kasesela: Mkishinda Uchaguzi msitamani wake za watu

Katika hatua nyingine, alimpongeza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Salim Abri Asas, kwa mchango wake mkubwa ndani ya chama hicho ambao umekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya chama hicho.

Aidha, alikipongeza chama hicho kwa ushindi wa asilimia 99.99 katika uchaguzi wa serikali za mitaa, akisisitiza kuwa CCM kimeshinda kwa haki na hiyo ndiyo sababu ya kutokuwepo malalamiko kutoka vyama vya upinzani.

Snapinsta.app_470902637_18331683742156445_7670009906499746146_n_1080.jpg
Snapinsta.app_470893884_18331683751156445_3226595737988344916_n_1080.jpg
 
Malalamiko kutoka vyama vya upinzani, kwani kuna vyama vya upinzani, akina mbowe, lipumba na cheyo ni wapinzani?
 
CCM hawahitaji raia wapige Kura wanahitaji polisi tu Kwa ushindi
 
Back
Top Bottom