GE2025 Kashakari: Nitahakikisha Kigoma kusini mnapata daraja Mto Malagarasi na Barabara ya lami

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Ahadi tulizozoea kusikiliza tukidanganywa kama hatuna fikra na kubaki kuwa ndoto kwa wananchi kutoka kwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi zinaendelea kwenye Kampeni Kigoma Kusini

-----------
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kupitia CCM, Nuru Kashakari maarufu Kandahari, amesema kipaumbele chake kikuu endapo atapewa ridhaa ya wananchi kuwa mbunge, ni ujenzi wa daraja la kitaifa lenye urefu wa mita 200 katika Mto Malagarasi, eneo la Ilagala

Amesema daraja hilo litakuwa na umuhimu mkubwa katika kuunganisha vijiji kiuchumi na kurahisisha upatikanaji wa huduma, ikiwemo kufikika kwa urahisi katika Hifadhi ya Taifa Mahalle. Ujenzi huo, kwa mujibu wake, utakwenda sambamba na ujenzi wa barabara ya lami yenye takribani kilomita 300 kutoka Simbo hadi Kalya

Kashakari ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi wa Kijiji cha Sunuka, ikiwa ni mkutano wake wa pili baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni zake Nguruka



Your browser is not able to display this video.
 
 

Attachments

  • 20250927_082957.jpg
    1.6 MB · Views: 29
  • 20250927_131106.jpg
    1.4 MB · Views: 27
  • 20250927_131024.jpg
    1.5 MB · Views: 26
Hili kivuko maragarasi ni hatari mnooo mnoo kwa matumizi.nilikua kua huko last week na hizo picha nimepiga mimi mwenyewe.

Kivuko kina jaaa maji,kinatembea huku ndani kuna water pump ya kumwaga maji mtoni.

Ni aibu sanaaa karne hiii binadamu kutumia kivuko cha aina hiii.


Kama haitakua hekaya ,wanaichi watafaidi matunda ya kodi wanazolipa

Ni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…