kashfa nzito necta watoa matekeo kwa mtu asie husika!

kashfa nzito necta watoa matekeo kwa mtu asie husika!

mwela

Member
Joined
Apr 26, 2011
Posts
47
Reaction score
7
MKURUGENZI GREEN ACRES
AFICHUA SIRI NZITO
na Betty Kangonga
WAKATI mjadala wa matokeo
mabaya ya kidato cha nne
ukiendelea kulitikisa taifa,
kashfa mpya ya matokeo hayo
imeibuliwa.
Kashfa hiyo mpya imeibuliwa na
Mkurugenzi wa Shule ya Green
Acres, Julian Bujugo, kwamba
matokeo ya baadhi ya shule
nchini ikiwamo yake
yamechakachuliwa.
Akizungumza na gazeti hili jana,
Bujugo alisema kuwa baadhi ya
wanafunzi kwenye shule yake
hawakufanya mitihani ya kidato
cha nne, lakini matokeo
yanaonesha wamefaulu kwa
kupata alama za juu.
Alitaja mfano wa mwanafunzi,
Humphrey Sanga, mwenye
namba 01197/148, ambaye
hakufanya mitihani hiyo lakini
matokeo yanaonesha amefaulu
kwa kupata alama nzuri.
“Huyu mwanafunzi
tulimsimamisha na hakufanya
mitihani, lakini matokeo yake
yanaonekana amepata hivi;
Civics D, Historia D, Jiografia C,
Kiswahili D, English C, Physics D,
Chemistry C, Biology C, Basic
Mathematics D, ambapo amepata
daraja la tatu pointi 24,” alisema
Bujugo.
Alimtaja mwanafunzi mwingine,
Martin Rushaigwa, namba
01197/0173, ambaye alifanya
masomo ya ‘Arts’.
Alisema matokeo ya
mwanafunzi huyo yanaonesha
kuwa ameongezewa alama za
masomo ya biashara ya
Bookeeping na Commerce,
ambayo hakuyafanya kabisa.
Alimtaja mwanafunzi mwingine
aliyefanya mtihani huo lakini
matokeo yake yanaonesha
amewekewa ‘absent’ na
mwanafunzi mwingine, Mbazi
Volta, hakufanya mitihani lakini
amepewa alama za ufaulu.
“Matokeo hayo yananipa
wasiwasi kwamba yanaweza
kuwa yamechakachuliwa,”
alisema Bujugo.
Mkurugenzi huyo anaiomba
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi kurudia kusahihisha
mitihani hiyo ili kuondoa
ukungu ulioligubika taifa kwa
sasa kuhusu matokeo ya kidato
cha nne.
“Naomba usahihishaji urudiwe,
maana huu ni ubabaishaji
mkubwa…matokeo hayo
yamewaathiri watoto
kisaikolojia na sijui watakwenda
wapi?,” alihoji.
Alisisitiza kuwa usahihishaji
urudiwe kwani katika shule hiyo
wanafunzi wenye uwezo
mkubwa tangu walipoanza
kidato cha kwanza ndio
waliofanya vibaya wakati
waliokuwa wakifanya vibaya,
wameibuka na alama za juu.
Mkurugenzi huyo alisema wazazi
wa watoto hao wanatarajiwa
kukutana mwishoni mwa wiki
hii kujadiliana kuhusu matokeo
hayo na hatua za kuchukua.
Akitolea ufafanuzi suala hilo,
Msemaji wa Baraza la Taifa la
Mitihani (NECTA), John Nchimbi,
alisema si kweli kuwa matokeo
hayo yamechakachuliwa bali ni
matokeo halisi ya shule hiyo.
Alisema iwapo mkurugenzi wa
shule hiyo ana shaka na
matokeo hayo, alitakiwa kufika
katika ofisi za baraza hilo ili
apatiwe taarifa sahihi kabla ya
kutoa taarifa katika vyombo
vya habari.
“Mi nimeangalia hayo majina,
naona yapo sawa na hata huyo
mwanafunzi ambaye
anasemekana hakufanya
mitihani na akapewa alama…
napenda kusema kuwa alama
alizopewa si zake na hata katika
orodha yetu anaonekana kuwa
hakufanya mitihani,” alisema.
Katika hatua nyingine, Waziri wa
wizara hiyo, Dk. Shukuru
Kawambwa na wenzake,
wamekuwa bubu kueleza
endapo wako tayari kujiuzulu au
la.
Tanzania Daima ilifika wizarani
hapo jana kutaka kuonana na
Waziri Kawambwa ili atoe
msimamo wake, mwandishi
alijibiwa kuwa waziri huyo
alikuwa kikaoni na asingeweza
kutoka.
Hata waziri alipopigiwa simu
pamoja na kutumiwa ujumbe
mfupi wa maneno, hakupokea
wala kujibu ujumbe huo.
Kwa upande wake, katibu mkuu
wa wizara hiyo naye hakuwa
tayari kuzungumzia suala hilo
kwa madai kuwa alikuwa
kikaoni.
Naye Naibu Waziri, Philipo
Mulugo, alipotafutwa kupitia
simu yake ya mkononi kueleza
msimamo wake, simu yake iliita
bila kupokewa na hata hakuwa
tayari kujibu meseji ya ujumbe
mfupi.
 
kazi ipo, inabidi kuanzishwa A level za kata inawezekana wafaulu ni wengi ila hawana pa kwenda.
 
NDO YALE YALE .TANZANIA HAINA VIONGOZI wa ELIMU WENYE VISION ya nini kifanyike ili kutoa huduma mtambuka kwenye nyanja ya elimu...Tutakaa na kusubiri sana,tena sana tu, kama vyeo ndo kwa staili hii ya kujuana na kubebana.
 
Back
Top Bottom