Eti kwenye hii kesi huyo mkuu wa wilaya alikuwa na haki ya kutetewa na ofisi ya mwanasheria mkuu?
huyu jamaa maneno ya shombo ndo yake
aliwahi kumwambia mtu 'asiwe anafikiria kwa kutumia tumbo' lol
yule si Masaburi??
Afu imekuwaje ukapost muda sawa na mie?
Wapi alisoma haijalishi ila kwa DC kutoa maneno kama hayo ni kudhihaki kiti chake. Aliyepiga walimu wazembe mkoani Kagera alifukuzwa kazi. Nashangaa kwanini Gumbo bado yuko ofisini.
KIkwete rais wa ajabu! Yaani hajamwajibisha huyu muhuni wake? Hata kama wanajuana walivyovuana chupi na kupeana shahada, Gumbo hakupaswa kuyasema aliyosema hadharani. Je katika mchezo huu rais anafaidika vipi? Je huu si ushahidi kuwa aliridhika na mwakilishi wake kumtukana bi wa watu? Ningekuwa huyu bi mkubwa ningemshitaki Gumbo na aliyemteua under vicarious accountability and liability.

Kosa la aliyemtuma ni kutomwajibisha anapoonyesha wazi kushindwa kufikia viwango ambavyo ni kuwahudumia wale waliomchagua aliyemwajiri kwa adabu na staha. Hii kwa kimombo huitwa vicarious accountability. Hili halina mjadala. Mwanao akiiba kama hutamchukulia hatua nawe unalaumiwa. Simple.
mkuu wa wilaya ya korogwe, mrisho gambo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya korogwe jana kwa shtaka la kumkashifu mwanasheria wa halmashauri ya mji korogwe kuwa ana stashahada ya chupi. Katika kesi hiyo, hakimu alikataa mwanasheria mkuu wa serikali kumwakilisha mkuu huyo wa wilaya katika kesi ya madai ya shilingi milioni 96 dhidi yake.
Katika kesi hiyo na. 7/ 2012 mlalamikaji ni mwanasheria wa halmashauri ya mji korogwe, najum tekka anayedai kukashifiwa na gambo wakati wa kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wilaya kwamba stashahada ya sheria aliyopata mtumishi huyo ni ya chupi.
Awali ilidaiwa kwamba mkuu huyo wa wilaya alimwalika mlalamikaji kutoa ushauri wa kisheria kuhusu namna ya kumaliza mgogoro baina ya halmashauri ya mji na wafanyabiashara na kwamba baada ya kufanya hivyo mlalamikiwa alipinga ushauri uliotolewa na kisha kutoa kauli hiyo kwamba shahada yake ni ya chupi.
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo hamis salum, mlalamikaji huyo aliiomba mahakama imwondoe mwanasheria mkuu wa serikali ambaye aliwakilishwa mahakamani hapo na wakili wa serikali, rebecca msalangi kwa kuwa hana mamlaka katika madai hayo na kamwe ofisi yake haikuwahi kupeleka ombi maalum la kutaka kumwakilisha gambo kwenye shauri hilo.
Jamani huyo Mkuu wa Wilaya amekosa nidhamu kwa kiwango cha juu. Bahati NZuri huyo Mwanasheria namfahamu saana, amesoma na kupata Shahada yake katika Chuo kikuu cha Tumaini huko Iringa!!!