Kashfa ya "degree ya chupi": Mkuu wa wilaya ya Korogwe kizimbani

Labda maoni yako yamesikilizwa.

Kwanini anasubiri wawe wengi kwenye fungu ndio achukue hatua? Amekuwa akifanya hivyo pia kwa mawaziri. Matokeo yake haionekani kama hatua au adhabu zimechukuliwa lakini pia kama mtu kasababisha damage basi ndio aendelee kuisabibisha mpk wakosaji wawe wengi? . Aliutaka urais wanini kama kuwawajibisha waliokosa kwake ni ngumu?
 
Kama chupi ni mbaya mbona ndio mnazitanguliza kuzivaa? mkuu wa wilaya teh teh teh we ni nomaaa!!
 
Lakini ni kweli TANZANIA degree za chupi ziko nyingi mno,,, ila sina uhakika na ya huyu...lakini anatakiwa aithibitishie mahakama kama alichokisema ni cha kweli!!!!
 
mkuu wa wilaya elimu yake hakuipata kwa njia ya chupi, sasa ande akapambane na mwanasheria aliyepata elimu yake kwa njia ya chupi.atakaeshindwa ndo huyo elimu kaipata kwa njia ya chupi.
 
Hapa mkuu wa wilaya ata takiwa athibitishie mahakama alikuwa ana sema ukweli.

Na huyo dada ata takiwa athibitishe hiyo ni kashfa sio ukweli.

Japo kwa haraka mkuu wa wilaya ana makosa ya kumdharisha huyo dada.

Tunataka kuona wanasheria wanakomaa mpaka kieleweke, maana kauli hiyo itawafanya wanasheria wengi wadharauliwe
 

Naona kama wanawake Tz hawana unity...

Nilitarajia suala kama hili lichukuliwe kwa uzito wa namna yake na jumuiya za wanawake nchini kushinikiza huyu mkuu wa wilaya awajibishwe na mamlaka za uteuzi wakati mahakama ikiendelea na kazi yake...

Ni aibu kwa WANAWAKE, hususani vyama na jumuiya za kutetea haki za wanawake kukaa kimya wakati mwanamke mwenzao akidhalilishwa kwa jinsi yake. Hili tusi sio mara ya kwanza kusikika katika jamii, na sioni ni kwa vipi waathirika (wanawake wasomi) wanathubutu kulifumbia macho na kukubali kuendelea kudhalilishwa...

TAWLA, TAMWA nk... mmenisikitisha sana....
 
Hata mimi nimesikitika sana. Hebu taasisi za wamama fanyeni kitu hapa. Mwenzenu anatukanwa tena kwenye kikao tusi ambalo hudhalilisha wadada siku zote halafu mpo kimya tu? Angetoa konda wa daladala tusi hilo wala nisingeumia, Mkuu wa Wilaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…