Sishangai kwa nini PM kajiuzulu kwa sababu kwa kila aliye na akili timamu alitegemea! mimi nafurahi tu!
Lakini nina wasiwasi kujiuzulu kwake kusije kukawa ni changa la macho kwa wa tz, tukasikie eti rais amekataa au hajajibu barua hiyo na kumlazimu huyu bwana kutengua uamuzi wake huku anajua ilikuwa geresha tu!!
Pili, sijui kama tunatakiwa kufurahi tu kwa kuambia PM kajiuzulu au baada ya kusikia kachukuliwa hatua zipi za kinidhamu na kisheria kwa kusaidia kuliingiza taifa kwenye matatizo makubwa, sijui sheria lakini naona kama hili linafanana sana na kosa la jinai!! Wenzetu kule ASIA kama China na Japan tumesikia tu mtu hasa viongozi akidhibitishwa kuhusika na rushwa ni kunyogwa!!
Naomba wa tz tusichekelee hatua hii pekee, bali tuangalia huyu bwana atachukuliwa hatua zipi ili liwe fundisho na kwa yeyote atakaye fuata hapo na viongozi wote kwa ujumla! Pia ripoti ya Mwakyembe imetoa mapendekezo ya kufanya mabadiliko kwenye taasisi kama TAKUKURU, Wizara ya Nishati, wizara ya fedha na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria wote walio husika kwa namna moja au nyingine kwenye mchakato wa kuipata RICHMONDULI!! Watu kama akina Arthur Mwakapugi, D.Yona, Karamagi na Msabaha na wote walio toa ushahidi wa wongo kwa kamati teule wachukile hatua kali kwa kukosa maadlili na uzalendo!!
Hivyo kwa maoni yangu tunacho taka kuona wana JF na watz wenye mapenzi mema, ni kwamba mapendekezo yote kwenye repoti ya Mwakyembe yamefanyiwa kazi!! HAPO NDIPO TUTAHEMA KWA FURAHA KIDOGO
festog