Kashfa zaendelea kumuandama Lacazette, Arsenal huenda ikampa adhabu nyota huyo

Kashfa zaendelea kumuandama Lacazette, Arsenal huenda ikampa adhabu nyota huyo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Arsenal wameapa kumwadhibu vikali mshambuliaji wao matata Alexandre Lacazette baada ya kuibuka kwa ripoti kwamba nyota huyo mzawa wa Ufaransa alipatikana akivuta gesi ya Nitrous Oxide almaarufu 'Laughing Gas' iliyokuwa imejazwa ndani ya puto.

Gazeti la Daily Star nchini Uingereza lilichapisha makala zenye picha zilizoonyesha Lacazette akiwa na puto lenye gesi hiyo mdomoni. Baadaye, mchezaji huyo wa zamani wa Olympique Lyon, Ufaransa aliwatumia wanasoka wenzake wa Arsenal video iliyochukuliwa akivuta gesi hiyo kupitia mitandao ya kijamii.

Ingawa msemaji wa Arsenal, ameshikilia kwamba tukio hilo ni "suala la kibinafsi" litakaloshughulikiwa na klabu katika kiwango cha "ndani kwa ndani", huenda Lacazette "akapata adhabu".

Ni wiki moja pekee imepita tangu Lacazette apatikane miongoni mwa wanasoka wengine wa Arsenal waliokiuka kanuni mpya za afya zinazodhibiti maambukizi zaidi ya virusi vya corona.

Lacazette, 28, alionekana akiwa karibu sana na mwanamume mmoja aliyekuwa akimwoshea gari lake jijini Londo, Uingereza.

Hivyo, alivunja kanuni inayotaka mtu kudumisha umbali wa hadi mita mbili kati yake na mwingine.
 
Haishauriwi kutumia hiyo gas bila kupewa ushauri wa kitabibu,ndio maana anatakiwa kupewa adhabu...
 
Ni vigumu sana kumkuta mchezaji mfaransa mstarabu...

Ukimuacha kante
 
Back
Top Bottom