Kashi kashi za simu

Kashi kashi za simu

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Ohoooooooooo, i am in trouble..plzz heeellllppp!! Tumekuchagulia mabinti wawili..uje uangalie yupi anakufaa uoe..mabinti wa huko mjini wahuni na matapeli tu...Ohoo..nifanyaje wadau??
 
Anakuja Bishanga kukushauri!, fanyia kazi ushauri wake!
 
oooooh it seems ur parents wants the best 4 u kataaa huwezi kuoa m2 usiempenda
 
Mara nyingi wazazi hujua weakness za watoto wao. Inawezekana mama ameona akusaidie katika hili. Kama unajiamini unaweza kujitafutia mwenyewe tafuta na umdhihirishie asiwe na was wasi na chaguo lako. Kama huna uwezo huo nenda kachague! pole!
 
Mmh...Huo mtihani mzitoo.. Vipi wewe kwani huna mpenzi?
 
Hivi unashindwa nini kumwambia mama yako sihitaji uniingilie kwenye mambo yangu binafsi mpaka unakuja huku kutaka ushauri?
 
Nadhani unajua wazazi wanavyoanza kuwaza baada ya kuona toto lao hali si mbaya sana...mh..mtihani huu..niuepukaje??? Sina mwanamke kwa sasa..
 
Hivi unashindwa nini kumwambia mama yako sihitaji uniingilie kwenye mambo yangu binafsi mpaka unakuja huku kutaka ushauri?

Mkuu inategemea na makuzi mzee, maza ni mzazi pekee niliyebakia nae..unafikiri hiyo ni njia sahihi ya kuepuka matakwa yake?? simply as that??? inahitajika njia sahihi bora na kutumia busara sio kukurupuka..wengine tumejifunza kuheshimu wazazi..inasaidia...Hata kwenye bible wameandika..usimdharau mama yako akiwa mzee..
 
kawapime oil kwanza ukiona wanafaa na kama hauna mtu mtu kwa sasa kama vip chagua moja,ukweli ndio huo wa mjini wengi matapeli tu
 
Ohoooooooooo, i am in trouble..plzz heeellllppp!! Tumekuchagulia mabinti wawili..uje uangalie yupi anakufaa uoe..mabinti wa huko mjini wahuni na matapeli tu...Ohoo..nifanyaje wadau??

Kama una mpenzi tayari, mwambie mama samahani tayari nina mchumba ila nitakuja kuongea na wewe kuhusu mpango wa ndoa, ila kama huna, wamekurahisishia kazi, nenda kaangalie kama wanakufaa na wana upeo wa kutosha kuishi na wewe na pia kama wana elimu japo ile ya awali!. Kumbuka kuwa upeo wa mwanamke ni muhimu sana anapohamia mjini vinginevyo atakuja kukutana na mapapaa na masharobaro akazibuka na kuanza kukusumbua.

Binafsi si-recommend kuoa kijijini kwa sababu ya mazingira, tamaduni, life style, norms, institutions nk kuwa tofauti mno na mjini kitu ambacho kinaweza kuchangia ndoa kutokudumu.
 
fanya kitu kimoja nenda huko ukiona hizo spicies hata mjini zinafit chukua goma ukiona miyeyusho waambie hujajipanga kuna mambo unayakamilisha yakishakaa sawa utawaambia kiroho safi..

:coffee:
 
Man nenda kachague mke,there is no need of thinking much,your mather knows what is good for u son.:whistle:
 
Kama una mpenzi tayari, mwambie mama samahani tayari nina mchumba ila nitakuja kuongea na wewe kuhusu mpango wa ndoa, ila kama huna, wamekurahisishia kazi, nenda kaangalie kama wanakufaa na wana upeo wa kutosha kuishi na wewe na pia kama wana elimu japo ile ya awali!. Kumbuka kuwa upeo wa mwanamke ni muhimu sana anapohamia mjini vinginevyo atakuja kukutana na mapapaa na masharobaro akazibuka na kuanza kukusumbua.

Binafsi si-recommend kuoa kijijini kwa sababu ya mazingira, tamaduni, life style, norms, institutions nk kuwa tofauti mno na mjini kitu ambacho kinaweza kuchangia ndoa kutokudumu.
.

Umenena mkuu..
 
we utakuwa ulijisahau , kama ungekuwa umeonesha una mwanamke hakuna mtu angehangaika kukutafutia mwanamke , nakushauri rudi chagua kifaa ambacho wamesha kutongozea oa endelea maisha, maana inaonesha ulikuwa hujiwezi kwenye sual la kutafuta mwanamka
 
Ndiyo maana wakakwambie uende ili ukachague lkn hawajakulazimisha sioni tatizo hapo.
 
Ha haaa nenda na wa kwako ulie naye town uenda naye huko kijijini kwenu uwapange kisha fanya gwaride kama la muswati ikibidi chagua yule wa kwako wa town hapo wazazi watapoa kidogo.
 
Kuwa makini sana ktk hilo!Make kama wengine walivyosema hapo awali,hawa wa hapa mjini wengi wao ni matapeli na wanapenda onyesha feki love mwanzoni! usije lia bila kupigwa na mifano hai ipo kibao tu humu jamvini.kama huna dem alie serious na ww,nenda kwa mama kawaone hao mabinti,kama utaona kuna anae weza kuwa tuned na kuishi nae mjini,bas jitwalie kilaini na tangaza ndoa! nadhan atakuheshim zaid na kkupenda!
 
stroke sioni kama mama yako amefanya vibaya, kibaya ni kukulazimisha mkuu. Si amakwambia kuna mabinti 2 kachague mmoja? We nenda kawaangalie, ukiridhika kubali uoe, usiporidhika unamwambia hujawapenda ,full stop. Mbona hata mimi wa kwangu nilimpata kwa njia hiyo hiyo, kwenda kumwangalia nikakuta yuko bomba, nikabeba mzigo hadi leo si-regret
 
kwa maana hiyo basi...ulilolisema ni ''trouble''?....

ninyi vijana ninyi....!haya jameni
 
Back
Top Bottom