Kasi Intaneti mpya kutoka Vodacom Plc

Vodacom Tanzania

Official Account
Joined
Aug 12, 2013
Posts
324
Reaction score
126
Vodacom Plc inafurahi kuwaletea KASI Intaneti, njia mpya ya kupata Intaneti isiyokata.

Ukiwa na KASI Intaneti unaweza kuperuzi, kutuma barua pepe, kuangalia filamu mtandaoni (yaani kustream), na kuendelea na biashara zako kama kawaida.
Intaneti hii inafaa kabisa kwa matumizi ya nyumbani na biashara ndogo bila kuwa na wasi wasi kuhusu Intaneti ya kutosha na kuendelea kutafuta fursa za kufanya biashara kama kawaida.

Unaweza pata Kasi Intaneti kwa 30GB, 60GB na 100GB, na zote hizi zinakuunganisha na intaneti yenye kasi. Utafurahia huduma ya Intaneti mpaka mwisho wa mwezi bila kukata.

Kujiunga na KASI intaneti ni rahisi, unachohitaji ni kununua router zinazopatikana kwa bei iliyo ya punguzo kwa ajili yako. Router hii itakuruhusu kuuanganisha watu hadi 25 na utaendelea kufurahia Intaneti kwa kasi ile ile bila kikomo.

Kupata maelezo zaidi kuhusu KASI Intaneti tembelea tovuti yetu hapa KASI INTERNET

Kujiunga na KASI Intaneti leo, tembelea Vodashop zilizopo jijini Dar es Salaam, Mbeya, Arusha au Mwanza na omba kuongea na Meneja au Mwakilishi wa Mauzo.
Pia unaweza kupiga 0766000673 au kutuma barua pepe kwenda vodacombiashara@vodacom.co.tz na tutawasiliana nawe kukusaidia ujiunge.

*Vigezo na Masharti kuzingatiwa *
 
modem 4g za ulaya ukirud nayo hom Tz itafanya kaz fresh!!
 
Mbona nikipiga io namba inasema namba unayopiga haipo na je hio router ni bei gani
 
Boresheni vifirushi vya simu wandugu,hizo kompyuta wanazo watu wachache sana ukilinganisha na simu.Mimi bado nipo na ombi hili maana ile ya Unit 50=dakika 1 bado ni mzigo mzito kwangu na kwa watu wa aina yangu.Pia Sh1000 kwa unit 300 /week au 500/ siku tatu ni gunia la misumali.Mmetuforce mpaka tunashindwa kuwasiliana na watu wa mitandao mingine.
 
Mi nataka munieleweshe kuhusu tuzo point ndo nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…