ReTHMI
Senior Member
- Jul 17, 2022
- 181
- 323
Uchumi wa nchi yoyote duniani hutegemea ni kwa namna gani viongozi wa nchi husika wanaongoza/wanatawala nchini mwao. Utawala wa viongozi ukiwa mbovu basi lazima kasi ya ukuaji wa uchumi iwe ndogo. Vilevile Utawala wa viongozi ukiwa bora/mzuri utapelekea ukuaji mzuri wa uchumi. Kwa maana hiyo basi, ukuaji mdogo wa uchumi wa nchi ni kiashiria tosha cha ubora mdogo wa viongozi katika kuongoza/kutawala.
Suluhisho la utawala mbovu ili kukomboa uchumi wa nchi
Nini kifanyike ili kuboresha utawala wa nchi?
1. Uwepo wa mkakati wa pamoja katika kutimiza malengo ya nchi.
Watafutwe wataalamu mbalimbali watakaokaa meza moja na kutengeneza mkakati mmoja utakaosaidia katika kutimiza malengo ya nchi. Nchi inayojengwa ni moja ni vizuri kutengeneza njia moja ya kufuata katika kutimiza malengo.
Itasaidia sana kiongozi mwingine anapoingia madarakani kuendelea pale alipoishia aliyetoka na sio kuanza upya na malengo yake. Nchi iachane pia na ilani ya vyama na kufuata malengo ya taifa yatakayoundwa na tume ya wataalamu. Itasaidia pia kujua nchi imefikia wapi kwa muda huo na itafikia wapi miaka kadhaa ijayo. Kwaiyo serikali husika iwe kwa ajili ya kusimamia kutimiza malengo ya nchi na sio ilani ya vyama.
2. Kutengeneza serikali ya mseto
Serikali ya mseto itamsaidia mkuu wa nchi kupata uwanja mpana katika kutafua wawakilishi bora wa kusaidiana nao katika uongozi. Serikali ya mseto itajumuisha viongozi kutoka vyama vingine vya siasa katika teuzi za mkuu wa nchi. Wapo watu wenye ubora mkubwa kwenye kila kigezo kinachohitajika katika nafasi fulani ya uongozi ila kutokana na kutokua chama tawala basi mkuu wa nchi anashindwa kuwateua kwenye nafasi za uongozi.
Pia serikali ya mseto itapunguza lawama kutoka kwenye vyama vingine pale inapotokea tatizo likasababishwa na utawala husika. Kwakua nao wanaunda utawala husika basi watashindwa kulaumu na kuamua kutoa maoni ni kwa namna gani ya kushughulikia hilo tatizo. Kwa maana hiyo nguvu ya kutatua tatizo itaongezeka na lawama zitapungua.
3. Kuwepo na uwazi katika mikataba wanayoingia viongozi wa nchi
Uingiaji wa mikataba uwe wa uwazi kwa nchi nzima mpaka upande wa wananchi wa kawaida. Hii itaepusha kwa wale viongozi wanaoingia mikataba mibovu kwa ajili ya masilahi binafsi au kutokana na ukosefu wa ujuzi/taarifa muhimu wa jambo husika kwenye mkataba. Pia kutokana na ukuaji wa teknolojia kwenye dunia ya sasa inarahisha katika kuwahusisha asilimia kubwa ya wananchi kuhusiana na masharti na faida za mikataba inayofanyika nchini.
Picha ya chini ikionyesha namna viongozi wanavyoingia mikataba mibovu kwa maslahi binafsi (kushoto) au kwa kukosekana kwa uelewa (kulia)
Chanzo cha picha: Masoud Kipanya
4. Mihimili ya nchi kueshimiana katika utoaji wa maamuzi
Mihimili ya nchi ijitegemee na kuachwa zitoe maamuzi yake bila kuingiliwa na mhimili mwingine. Mahakama zitoe maamuzi kulingana na sheria za nchi na sio kulingana na maelezo kutoka sehemu fulani. Pia maamuzi ya bunge yafanywe bila kuingiliwa uhuru wake. Hivyohivyo kwa upande wa mkaguzi mkuu wa serikali afanye kazi yake kwa ufanisi bila kuingiliwa uhuru wake. Hii itapelekea mihimili ya nchi kufanya kazi kwa uhuru na sio kwaajili ya masilai ya mtu mmoja au kikundi fulani cha watu serikalini.
5. Sheria za nchi ziboreshwe (zirekebishwe)
Viongozi waondolewe kinga za kutoshtakiwa pale watakapobainika walivunja sheria za nchi. Itasaidia kupata viongozi watakaotumia vizuri rasilimali za nchi kwa manufaa ya nchi husika na pia watakaoheshimu sheria za nchi. Hii ni kutokana na kutambua kwamba watakapovunja sheria za nchi au kufanya ufujaji wa rasilimali za nchi kwa masilahi binafsi basi watahukumiwa kama wahalifu wengine pindi watakapotoka au watakapotolewa madarakani.
Pia kwa viongozi watakaobainika kufuja mali za umma au rasilimali za nchi kwa masilahi binafsi basi wachukuliwe hatua kali. Kulipa fidia na kutenguliwa nafasi yake hakutoshi kua fundisho kwa wengine. Ikiwezekana ziwepo sheria za vifungo jela na kufilisiwa mali zao, hii itasaidia viongozi kusimamia vizuri mali za umma na rasilimali za nchi bila tamaa binafsi.
6. Tume huru ya uchaguzi
Uhuru wa tume ya uchaguzi utatokana na njia zilizotumika kuwapata viongozi wa tume husika. Ni ngumu sana kwa kiongozi wa tume ya uchaguzi kutokupendelea upande wowote ilihali aliyempa hiyo nafasi naye anashiriki kwenye uchaguzi. Ni sawa na mfanyakazi kumkataa bosi wake huku akibaki na wasiwasi wa kibarua chake.
Uundaji wa tume ya uchaguzi uwe wa huru ili isaidie kuhalalisha viongozi waliopitishwa na wananchi. Na sio kuhalalisha viongozi ili kujilindia nafasi walizonazo.
7. Matumizi na malipo kwa viongozi yaendane na uchumi wa nchi
Uchumi wa nchi unajumuisha pato la mtu mmoja mmoja kwenye nchi husika. Inapotokea uchumi wa mtu mmoja mmoja kwenye nchi upo chini lakini malipo ya viongozi yapo juu basi watu wengi wataingia kwenye siasa kwa ajili ya kutafuta nafasi ya uongozi kutokana na tamaa ya pesa. Hii itapelekea kupata viongozi wasio wazalendo na wasio na uwezo wa kuongoza ila kupata nafasi kutokana na nguvu za ushawishi walionayo (wasanii wakubwa, watu maarufu na wafanyabiashara wakubwa) wanaohitaji nafasi hizo kutokana na tamaa ya pesa.
Lakini malipo yakiwa ya kawaida yanayoendana na uchumi wa mtu mmojammoja, taifa litapata viongozi wazalendo wasio na tamaa ya pesa wenye nia njema na nchi.
8. Kufuatilia na kufanyia kazi ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)
Ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali itakapobainisha dosari yoyote kwenye sekta serikalini basi hatua zichukuliwe. Sheria zichukuliwe kwa wale watakaobainika kufanya ufujaji wa fedha za serikali. Pia maboresho na marekebisho yafanyike ili kupunguza dosari kwenye mwaka mwingine wa fedha.1. Uwepo wa mkakati wa pamoja katika kutimiza malengo ya nchi.

9. Wananchi wapewe uhuru wa kuwasilisha maoni yao
Viongozi wengi wa nchi wanashindwa kutambua kwamba nguvu ya serikali ipo kwa wananchi. Kumekua hadi na baadhi ya maneno yasiyofaa kutoka kwa viongozi kwenda kwa wananchi kutokana na wanachi kulalamikia badhi ya njia zinazoonekana kuwaumiza. Kwa uongozi ulio bora inapaswa kuwasikiliza wananchi pale wanapotolea maoni jambo fulani. Njia hii itasaidia kuzuia njia za kuongoza nchi zinazowaumiza wananchi walioichagua serikali hiyo. Mwanchi akisikilizwa inampa nguvu ya kusimamia na kushiriki katika maendeleo ya nchi.
Hivyo basi, utawala bora ni suluhisho la ukuaji wa uchumi kwenye nchi. Na utawala bora unatokana una ubora uliopo katika sekta zote za serikali. Sekta moja ikiyumba basi ni rahisi kuyumbisha utawala mzima pia. Ifike wakati viongozi wote watambue wanachopambania ni uchumi wa nchi na sio masilahi binafsi (uchumi wao binafsi).

Upvote
3