Kasi ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa UKIMWI katika Jiji la Tanga Imeshuka kutoka asilimia 5 mpaka 2.2

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
KASI ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi katika Jiji la Tanga yameshuka kutoka asilimia tano mwaka juzi hadi asilimia 2.2 Julai mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Ukimwi wa Jiji la Tanga, Mosses Kisibo wakati akiongea na gazeti hili kuhusu mikakati ya utekelezaji wa shughuli za ugonjwa huo kipindi cha mwaka huu.

Kisibo alisema kupungua huko kunatokana na hamasa ya elimu ya upimaji wa hiari waliyoitoa kwa jamii kuanzia ngazi ya shule za msingi.

“Kutokana na elimu ya upimaji wa hiari kuwafikia wananchi wengi, sasa kasi ya watu kujitokeza kupima imeongezeka kutoka watu 51,344 mwaka 2017 hadi kufikia watu 66,308 mwaka 2018,” alisema Kisibo.

Hata hivyo ili kuwalinda vijana na tabia hatarishi zinazosababisha maambukizi, Kisibo alisema wameshaanza kupeleka elimu ya mafunzo ya mifumo ya ustawi wa jamii na maswala ya Ukimwi kwa shule za msingi 15 na za sekondari 12 ndani ya jiji hilo.

Alisema miongoni mwa vyanzo vya ueneaji wa ugonjwa huo ni vitendo vya ukatili wa kingono, hivyo iwapo elimu itawafikia wanafunzi hao wataweza kujikinga dhidi ya vitendo hivyo na maambukizi.

Vile vile akiongelea uanzishaji wa dawa za kufubaza virusi vya ugonjwa huo, alisema kuwa wamefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 91 kuwaingiza katika matumizi ya dawa za ARVS waathirika hao.

Kwa upande wake, mratibu wa mradi wa afya kamilifu unaotekelezwa na Shirika la Amref, Dk. Edward Kilimba, alisema kuwa wamefanikiwa kupeleka bajeti ya Sh mil 158 kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga ili kutekeleza miradi ya Ukimwi maeneo kinga, tiba na kuboresha mifumo ya utoaji takwimu.

“Tunaamini iwapo tutaweza kuwajengea uwezo wataalamu wa afya katika eneo la takwimu, wataweza kujua kwa haraka kama mikakati ya kupambana na ugonjwa huo inafanikiwa au laa,” alisema Dk. Kilimba.
 
Mmmmh!!! Mkuu habari hii itafungulia mwendo kasi leo jijini
 
Yaani nazidi kujiimarisha kiimani kuwa hakuna ngoma, yaani mapenzi yote kule Tanga maambukizi yameshuka? Ntaendelea kugonga bila ndomu aisee
KASI ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi katika Jiji la Tanga yameshuka kutoka asilimia tano mwaka juzi hadi asilimia 2.2 Julai mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Ukimwi wa Jiji la Tanga, Mosses Kisibo wakati akiongea na gazeti hili kuhusu mikakati ya utekelezaji wa shughuli za ugonjwa huo kipindi cha mwaka huu.

Kisibo alisema kupungua huko kunatokana na hamasa ya elimu ya upimaji wa hiari waliyoitoa kwa jamii kuanzia ngazi ya shule za msingi.

“Kutokana na elimu ya upimaji wa hiari kuwafikia wananchi wengi, sasa kasi ya watu kujitokeza kupima imeongezeka kutoka watu 51,344 mwaka 2017 hadi kufikia watu 66,308 mwaka 2018,” alisema Kisibo.

Hata hivyo ili kuwalinda vijana na tabia hatarishi zinazosababisha maambukizi, Kisibo alisema wameshaanza kupeleka elimu ya mafunzo ya mifumo ya ustawi wa jamii na maswala ya Ukimwi kwa shule za msingi 15 na za sekondari 12 ndani ya jiji hilo.

Alisema miongoni mwa vyanzo vya ueneaji wa ugonjwa huo ni vitendo vya ukatili wa kingono, hivyo iwapo elimu itawafikia wanafunzi hao wataweza kujikinga dhidi ya vitendo hivyo na maambukizi.

Vile vile akiongelea uanzishaji wa dawa za kufubaza virusi vya ugonjwa huo, alisema kuwa wamefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 91 kuwaingiza katika matumizi ya dawa za ARVS waathirika hao.

Kwa upande wake, mratibu wa mradi wa afya kamilifu unaotekelezwa na Shirika la Amref, Dk. Edward Kilimba, alisema kuwa wamefanikiwa kupeleka bajeti ya Sh mil 158 kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga ili kutekeleza miradi ya Ukimwi maeneo kinga, tiba na kuboresha mifumo ya utoaji takwimu.

“Tunaamini iwapo tutaweza kuwajengea uwezo wataalamu wa afya katika eneo la takwimu, wataweza kujua kwa haraka kama mikakati ya kupambana na ugonjwa huo inafanikiwa au laa,” alisema Dk. Kilimba.
 
Hizi ni promo walahi, mabinti wa kitanga walikuwa wamefunikwa kwenye headlines.... hapa wataanza kutrend upya.
 
Back
Top Bottom