Kasi ya utendaji wa Rais wa awamu ya tano inawabeba watendaji wake wengi mno na ni hatari sana wakibweteka

Malimu Nyerere aliwahi kusema.
"Ukitaka kumsaidia Maskani si kuwapanga na kuwagawia pesa ila somesha Mtoto wa maskini tena mpe elimu nzuri"
Hii falsafa ni nzuri sana kwa sababu ukisha mpa mtoto elimu nzuri, kwanza huwezi kumnyang'anya na pili hii elimu itasaidia wazazi wake na Taifa.
Kuna vitu vizuri sana anafanya Rais wetu na ambavyo viongozi wanaokuja kumridhi kama watakuwa wabovu vituo vya afya vitabaki majengo matupu yasilyo na dawa wala wataalamu, elimu ya bure haitakuepo, mabara bara hayatatengenezwa yaharibika b nk.
Tuendelee kuboresha elimu ya watoto wetu ili iwe bora na baada ya hapo basi huyu mtoto wa maskini apate ajira.
Huwezi kusema ajiajiri kwa sababu anakuwa hana mtaji na uzoefu.
 
Wameisha bweteka unategemea kubweteka mara ya mpili.Yule kijana wa Munauye Moses alipowatetea wapiga kura wake wakulima wa korosho wapo wenzake waliomubeza lakini jamani ni wabunge wa aina gani wanaopewa kura wakienda bungeni hawatetei wapiga kura wake wanaishia kuunga mkono ,hawathubutu kuuliza yale magumu yanayowaumiza wakulima,wafanyabiashara,watumishi wa umma wanaishia kugonga meza na kubeza yule anayewapinga bila kuwatetea kikamilifu wapiga kura wao.
 
ukosefu wa ajira , utekaji , kuondoa nyongeza ya mishahara , kula hela ya Tetemeko , kuua demokrasia na kuneemesha Chatto huo ndio utendaji ?
 
Eti kasi ya utendaji, propaganda za kishamba tu.
Kukataa ukweli haimaanishi haupo Mkuu....kama upo upo tu.
Yapo mazuri yanayoonekana waziwazi na ndiyo hayo yameoneshwa hapo udhaifu wa Kibinadamu kila mmoja anao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…