Kasim Majaliwa: Sensa itafanyika kielekroni na tuna uhakika litafanikiwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wakuu, nipo Dodoma kwenye kongamano la Tathmini na Ufuatiliaji lililoratibiwa na Tanzania Evaluation Association.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema zoezi la anuani za makazi limefanikiwa kwa 85% na amesema zoezi la sensa litafanyika kielektronik hadi huko kijjijini. Japo sijaelewa ni namna gani iliyopo ambaye inatajwa kuwa ni ya kielektronik.

Kikubwa ameshaaga, ndio anaondoka sisi tuendelee na kongamano.
 
Hata 2025 tupige kura kielectronic
 
Tena huyo sio wa kumuamini. Ilo zoezi ya anuani za makazi namba za nyumba zimeishia kuandikwa na chaki. Bado kuna serikali za mtaa zinatumia mwanya kutoza pesa za vibao
 
Watatumia tablets kuingiza data..sio makaratasi tena..taarifa zitafika makao makuu siku hiyohiyo na kuanza kufanyiwa kazi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wakuu, nipo Dodoma kwenye kongamano la Tathmini na Ufuatiliaji lililoratibiwa na Tanzania Evaluation Association.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema zoezi la anuani za makazi limefanikiwa kwa 85% na amesema zoezi la sensa litafanyika kielektronik hadi huko kijjijini. Japo sijaelewa ni namna gani iliyopo ambaye inatajwa kuwa ni ya kielektronik.

Kikubwa ameshaaga, ndio anaondoka sisi tuendelee na kongamano.
Shida yangu ni kama mtu wa kawaida anaweza kujibu dodoso mwenyewe na kujaza, watakao fanya scripting watumie programme rafiki kwa mtu wa kawaida asiejue lolote kuhusu kujaza na kujibu maswali kwenye dodoso, na pia dodoso lisiwe refu sana, sijajua kama vijiji vyetu vyote vina mtandao wa simu mzuri unaoweza kuupload na kushusha dodosa kwa muda unaotakiwa na sidhani kama kila mtu huku Litapwasi kama ana simu janja, na je hela ya bundle kwa ajili ya kushusha na kutuma itatoka wapi, je kila simu itakuwa na uwezo wa kupokea hilo dodoso, kifupi kunatakiwa elimu zaidi, hili la makazi tunatumiwa tu meseji kwenye simu na ukibofya inaonyesha eneo la mtaa tu je vipi kuhusu namba za nyumba, huku kwetu tumeandikiwa namba ukutani/mlangoni na hata walioandika hatujawahi kukutana nao na hatujui hizo namba ni zanini?hata fomu hatujawahi kuziona!
 
Bado kuna sehemu nyingi sana hilo zoezi la anwani za makazi halijafika kabisa. Kuna sehemu zingine limeishia njiani-barabara/makazi hazijafikiwa hadi leo
 
Wakuu, nipo Dodoma kwenye kongamano la Tathmini na Ufuatiliaji lililoratibiwa na Tanzania Evaluation Association.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema zoezi la anuani za makazi limefanikiwa kwa 85% na amesema zoezi la sensa litafanyika kielektronik hadi huko kijjijini. Japo sijaelewa ni namna gani iliyopo ambaye inatajwa kuwa ni ya kielektronik.

Kikubwa ameshaaga, ndio anaondoka sisi tuendelee na kongamano.
Bahasha yake imewekewa shs ngapi?
 
Back
Top Bottom