MURUSI
JF-Expert Member
- Jun 25, 2013
- 4,537
- 8,824
Zamani ulikuwa huwezi taja kilimo bila kuitaja Kaskazini, mkoa kama Arusha na nazania Arusha ndio ilikuwa kituo cha kilimo Tanzania hii, Kaskazini hasa Arusha ndiko hata kulikuwa na Makao makuu ya TFA, makampuni makubwa ya mbegu yote ni Arusha na taasisi zingine.
Pia kwenye Kilimo hasa Mahindi, Ngano/Shayri, mboga mboga na Kahawa na ndizi huko ndio ilikuwa kwao.
Ila kwa miaka ya hivi karibuni naona kabisa kaskazini hasa Arusha ikiwa haifai tena kwa Kilimo kama zamani.
Ukame ikiwa ni moja ya sababu kubwa sana kwa sasa, Arusha na mikoa mingine kama Kilimanjaro na Manyara zina ukame usio isha, na sioni Dalili za hali kuja kuwa nzuri tena. Kuna Ukame mrefu sana kaskazini na bahati mbaya hakuna hata mito mikubwa ya kutumika kwa Irrigation kama mikoa mingine.
Bei kubwa ya Ardhi, kaskazini Ardhi ni ghari mno, kiasi kwamba unahitajika kuwa vizuri mno kupata shamba huko Kaskazini jamaa wali jua thamani mapema sana.
Ardhi ni chache ni haba sana kwa sasa, Ukitoa wilaya kama mbili za Kaskazini yaani Simanjro na Kiteto hakuna tena sehemu unaweza mapata mashamba kwa huko kaskazini.
Watu wanchache wana hodhi ardhi kubwa sana, Kaskazini kuna Mastle kama wale wa Zimbabwe, wana milik hekari za kutosha za Ardhi na hii inapelekea uhaba na bei kuwa juu sana.
Kwa anaye fanya kilimo simshauri huko kaskazini kwakweli binafisi napaona hapafai kabisa kwa sasa.