Pre GE2025 Kaskazini Pemba: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Mkuu 2025

Pre GE2025 Kaskazini Pemba: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Pemba Kaskazini.jpg

Misamiati:
Baraza: Wilaya
Wadi - Kata

Mkoa wa Kaskazini Pemba ni moja kati ya mikoa 31 ya Tanzania, unapatikana Kaskazini mwa Kisiwa cha Pemba, huko Zanzibar.

Mkoa wa Kaskazini Pemba una Halmashauri mbili (2) na majimbo ya uchaguzi tisa (9) ambapo Jimbo la Kojani linaongoza kwa kuwa na watu wengi 36,917, likifuatiwa na Jimbo la Micheweni lenye watu 35,567.

Majimbo ya Kaskazini Pemba ni pamoja na;
  1. Gando
  2. Wete
  3. Pandani
  4. Kojani
  5. Mtambwe
  6. Micheweni
  7. Wingwi
  8. Konde
  9. Tumbe
Hali ya Kisiasa

Katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kushinda katika majimbo matano kati ya tisa, ambayo ni Gando, Kojani, Micheweni, Wingwi, na Tumbe, kwa kupata asilimia kubwa ya kura. Kwa ujumla, CCM ilipata takriban 45% ya ushindi katika mkoa huu.

ACT-Wazalendo nayo ilijipatia ushindi katika majimbo matatu, ambayo ni Konde, Wete na Mtambwe. Ushindi huu umeiweka ACT-Wazalendo kama chama chenye nguvu kubwa katika mkoa huu, ingawa CCM bado imeendelea kuonyesha ushindani wa karibu.

Vyama vingine kama CHADEMA, CUF, na ADC vilipata asilimia ndogo sana ya kura zilizopigwa, kwa ujumla havikuonyesha ushawishi mkubwa katika Mkoa huu.

Ingawa CCM ilishinda uchaguzi huo kwa asilimia kubwa, matokeo yalizua malalamiko makubwa kutoka Vyama Vya Upinzani, ambapo ilidaiwa kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.

Maandamano na machafuko yalitokea baada ya uchaguzi, huku jumuiya za kimataifa zikikosoa mchakato wa uchaguzi na mwelekeo wa demokrasia visiwani Zanzibar. Serikali ya CCM ilikataa tuhuma hizo na kuendelea na utawala wake.

Soma, Pia:
Januari
 
Back
Top Bottom