ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitoa msimamo huo bungeni Dodoma jana kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa hapo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Janet Mahawanga (CCM).
Mbunge huyo alitaka kufahamu ni lini serikali itaboresha sheria za uhamiaji ili kuweka urahisi kwa wawekezaji wa kimkakati kupata uraia kutokana na heshima ya uwekezaji wao kwa taifa kama wafanyavyo mataifa mengine.
Majaliwa alisema serikali inawapa fursa wawekezaji hao ahueni ya kikodi, kibiashara na kuwapa ushirikiano katika uendeshaji na wanapoishi kwa miaka 10 wanapata nafasi ya kuomba uraia.
“Mradi tu anapopata uraia, lazima akubali kuendelea kuwa Mtanzania, lakini pia awe miongoni mwa watu wanaochangia uchumi na hayo yote yanapofikishwa uhamiaji hakuna shida kwa sababu wanasimamiwa na TIC (Kituo cha Uwekezaji Tanzania),” alisema.
Majaliwa alisema serikali ina mifumo na sheria za uhamiaji kama nchi nyingine na kwamba sheria zinaruhusu watu kutoka nje kwa vibali maalumu na shughuli mbalimbali.
Alisema uwekezaji wa kimkakati hauwezi kuwa wa mwaka mmoja, miwili, mitatu au minne hivyo wawekezaji wa miaka 10 ni wale ambao wameishi nchini kwa muda mrefu na wanahitaji uraia.
“Tunapojiridhisha huyu ni mwekezaji wa mradi mkubwa wa gharama kubwa na wa muda mrefu, wanahitaji usimamizi wa karibu, hao nao tumewafungulia dirisha lao la kuona umuhimu wa wao kuwa sehemu yetu,” alisema Majaliwa.
===
My Take
Ndio hivyo, ukiwa na pesa unabembelezwa kama vile wachezaji wenye vipaji wanavyopembelezwa kuchezea Mataifa mbalimbali.