Nawasalimia kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Unaposikia duniani kuna mengi, kweli mengi yapo. Mengine ni ngumu kuyapatia ufumbuzi hususa kwa akili ya kawaida ya kibinadamu inapotumika.
Kwa sababu kuna matukio ambayo huwaga yanatokea inakuwa ngumu kuyaelewa labda uwe na nguvu ya ziada ya kiMungu au kishetani.
Wale waliokulia kwenye familia za kimasikini pamoja na vijijini wamewahi kukumbwa na tatizo la chawa, na pia kuna baadhi ya maeneo hususa kipindi cha nyuma ambayo ilisharipotiwa kuwa na chawa wengi sana, lakini pia hata sasa wale ambao hawazingatii usafi wa nguo wanaweza wakapata chawa.
Katika Hali ya kushangaza kuna tukio moja limetokea katika Kijiji cha Kabanga halmashauri ya mji Kasulu - Kigoma 30/4/2021 asubuhi, chawa wengi mno kuonekana darasani.
Msimuliaji anasema katika darasa hilo, siku ya Jana yake jioni darasa limefanyiwa usafi vizuri na wanafunzi maana lilikuwa linaandaliwa kwa ajili ya mtihan na pia ndoo darasa hilo linalotumika siku zote na darasa 7.
Anaendelea kusema, wanafunzi kama kawaida waliingia darasani asubuhi mmoja ya wanafunzi akakuta kuna kama kichuguu kikubwa cha chawa kimetengenezwa ndani karibu na sehemu anapokaa, akajaribu kukigusa basi hapo ndoo ikawa shughuli, wale chawa walisaambaa darasa zima ikabidi wanafunzi waanze kupiga makelele huku wakikimbia nje.
Ndipo walimu wakaja wakakuta chumba kizima kimejaa chawa, madaftari ya wanafunzi yamejaa chawa, na baadhi ya wanafunzi wameshapata chawa hali ambayo watu walishindwa kuielewa kwa sababu kila mmoja alizungumza la kwake. Kutokana na Hali hiyo ilibidi darasa zima lipuliziwe dawa ili kuwaua chawa. Ni tukio ambalo limekuwa gumzo kijijini hapo.
Wataalamu wa Mambo mtusaidie hilo tukio unaweza ukalielezaje? Maana watu humu JF tunatofautiana. Kina Mshana jr na wengine karibuni sana.
Naomba kuwasilisha.