Kata Funua Aliyopigwa Simba SC pale Kwa Mkapa na Makhirikhiri, Mo Dewji Alaumiwe?

Kata Funua Aliyopigwa Simba SC pale Kwa Mkapa na Makhirikhiri, Mo Dewji Alaumiwe?

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Mnaweza Kuwalaumu Wachezaji, lakini kwa ubora ule wa wakina Sakho, Kanoute na Banda ni vigumu sana kwa mtu mwenye akili kichwani kutarajia makuu kutoka kwao.

Mnaweza kumlaumu kocha lakini kwa wachezaji alioletewa na Mo Dewji...anakosewa heshima. Licha ya kuwa Didier GOMES sio mwalimu mwenye ufundu sana kama Prof Nabi. Ni aina fulani ya makocha ambao wanategemea kuletewa wachezaji wazuri ili asitumie akili zake nyingi kuleta matokeo.

Aliye sababisha kiwango na ubora wa Simba SC kudidimia kiasi hiki ni yule ambaye mnamuogopa hata kumnyanyulia mdomo, ati kwa sababu analipa mishahara wachezaji.

Yes, ni huyo huyo ambaye ameingiza mpunga mrefu kwa mauzo ya wakina Chama & Miqquesone akaamua kuzipeeka pesa zote kwenye mashamba yake ya michai chai huyo Mbeya wilayani Rungwe.

Yes, ni huyo huyo ambaye hafanyi uwekezaji mkubwa wa kifedha klabuni na badala yake yakutokea yakitokea anaanza kutafuta mchawi ni nani ndani ya Klabu.

Mo Dewji ni MCHAWI. Amini ninalo waambia.
 
Mo Dewji kasusia timu tangu auze Chama na Miquissone, alijua alichofanya ila sasa anajifanya kuumizwa na kutoa ushauri. Kumbe anawang’ong’a wenzie.
 
Mo kuuza chama na Luis ni sawa na mtu kuchukua chake mapema,kashachukua chake mda c mrefu anakula mita anaacha timu.
 
Back
Top Bottom