Arch - Forum Tz
Member
- Sep 20, 2019
- 15
- 35
Katika jamii zetu yapo makundi Mbalimbali ambayo yanakumbwa na unyanyasaji, Ubaguzi pamoja na ukatili. Licha ya kuwa wapo watu wengi ambao wankumbwa na hali hiyo ila nitajikita katika makundi maalumu. Makundi hayo yapo katika mgawanyo huu:
Wanawake
Walemavu
Wazee na
Watoto
Makundi haya kila kundi linachangamoto yake na nitagusa kundi moja na changamoto yake na jinsi ya kuzitatua.
Wanawake:
Hili ni kundi ambalo hukumbwa na ukatili na unyanyasaji wa namna Mbalimbali, mara nyingi wananyanyaswa kingono na waajiri majilani au watu wasiojulikana, Waume zao kuwapiga, Kunyimwa mirathi, kubakwa, mimba zisizotarajiwa, Kufukuzwa shule kwa watoto wa kike wakipata ujauzito, kufanyiwa ukeketaji na wakati mwingine hata makundi ya kijamii kama dini kuwatenga na kuwanyima ushiriki katika jamii.
Ili kulisaidia kundi hili ni lazima kufanya yafuatayo:

- Elimu ya jinsi na jinsia itolewe katika jamii, taasisi za elimu na viundwe vikundi maalumu ili kutoa elimu kwa wanawake.
- Serikali iboreshe na kusimamia sheria zinazolinda haki ya mwanamke ikiwa ni pamoja na kuwaruhusu wanawake wanaopata ujauzito kuendelea na masomo baada ya kujifungua.
- Tasisi za dini zibadili mtazamo wake kuhusu wanawake na kuwaruhusu kushiriki katika shughuli Mbalimbali zakijamii.
Walemavu:
Kundi hili linajumuisha watu wote ambao wanaupungufu au hitilafu la kudumu katika mwili au akili zao. Unaweza kuwa ulemavu wa viungo, ngozi au akili.
Changamoto kubwa wanayokutana nayo walemavu ni kubaguliwa, baadhi ya jamii huwaua walemavu wa ngozi (albino) kutokana na imani potofu hasa za kishirikina. Vilevile Walemavu wengi hukosa msaada kutoka serikalini na kwenye jamii ikiwemo vitendea kazi na hivyo kuishi maisha ya shida.
Ili kulisaidia kundi hili ni lazima kufanya yafuatayo:
- Jamii inapaswa kuondokana na imani potofu kuhusu walemavu hasa imani za kishirikina, kwani imani hizo hazina ukweli wowote.
- Kuanzisha vituo maalumu vya kulelea watoto wenye ulemavu nchi nzima.
- Kuanzisha shule nyingi za watu wenye ulemavu.
- Kutoa Elimu kwa jamii kuhusu wajibu wa raia katika kuwatunza walemavu na haki zao za msingi kama raia wengine.
- Kuboresha na Kusimamia sheria ipasavyo ili kuwalinda watu wenye ulemavu.
Wazee na Watoto:
Kundi hili nimeliweka pamoja licha ya kuwa ni makundi mawili tofauti lakini wenye uhitaji na changamoto zinazofanana.
Kundi hilo la wazee na watoto changamoto kubwa inayowakabili ni Kukosa uangalizi na vifo. Mara nyingi wazee na watoto wanauawa na kunyofolewa viungo vyao kutokana na imani potofu na Kukosa masaada. Kukosa ungalizi kwa wazee na watoto kunaongeza ombaomba na watoto wa mtaani.
Ili kulisaidia kundi hili yafuatayo yanatakiwa kufanyika:

- Selikali kuanzisha Taasisi maalumu na imara ambayo itawasaidia wazee ambao hawana uangalizi au ndugu wa kuwasaidia.
- Jamii kuachana na mila na imani potofu ambazo husababisha vifo vya wazee na watoto.
- Kuongezwa kwa vituo vya kulelea watoto yatima nchi nzima.
- Serikali kuweka vipaumbele katika makundi haya ikiwa ni pamoja na kuwaingiza katika mpango wa kudumu wa kuwsaidia.
Hitimisho, Serikali na jamii zote zinao wajibu wa kuhakikisha makundi yote maalumu yanapata haki zote bila kubaguliwa wala kupata kipingamizi chochote ili kuwajengea mazingira rafiki watu wote wanaopatikana katika makundi hayo. Sheria inasema, "watu wote ni sawa".
Upvote
1