‘Kataa Ndoa' Inavyotishia Maadili ya Familia na Jamii: Mabadiliko ya Kijamii Duniani ya Athari Zake

‘Kataa Ndoa' Inavyotishia Maadili ya Familia na Jamii: Mabadiliko ya Kijamii Duniani ya Athari Zake

Tape measure

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2015
Posts
1,981
Reaction score
3,604
Tatizo la upungufu wa nguvu kazi linazidi kuwa kubwa duniani, na halikuwa tatizo la ghafla bali linatokana na mabadiliko ya kijamii na kisiasa ambayo yamekuwa yakijitokeza kwa muda mrefu. Kwa mfano, Urusi mwaka huu 2024 imeanzisha sera za kutoa motisha kwa wanawake kuzaa watoto, ikiwa ni pamoja na faida za kifedha kwa akina mama na ahadi ya msaada wa serikali kwa familia. Hata hivyo, tatizo bado linajitokeza kwa sababu vijana wengi wanachagua kuwa na maisha ya Ubachela/single, kazi na anasa, au kukumbatia wazo la kutokuwa na watoto na familia.

Nchini Japan, tatizo la kupungua kwa idadi ya watu linajitokeza kwa kiasi kikubwa. Serikali imeanzisha mikakati mingi ya kusaidia jamii kuanzisha mahusiano na ndoa, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa waziri wa "Upweke" ili kushughulikia tatizo la kujitenga kwa watu kutoka kwa jamii. Licha ya jitihada hizi, kiwango cha uzazi kinapungua kila mwaka, na idadi ya watu wanaoishi katika hali ya HIKIKOMORI—ambao ni vijana wanajitenga na jamii kwa miaka mingi—inaongezeka. Watu hawa ni zaidi ya milioni 2 sasa, na wengi wao hawajawahi kuanzisha mahusiano ya kimapenzi wala kufanya mapenzi, jambo linaloleta changamoto kubwa kwa jamii.

Korea Kusini pia ilikumbwa na wimbi kubwa la FEMINISM ambalo lilichochea wanawake kupigania haki zao. Slogani maarufu “4N” (NO MARRIAGE, NO SEX, NO BIRTH, NO RELATIONSHIP) ilikubalika kwa vijana wengi, msemo huo ulitumika mpaka na wanasiasa kwenye kujizolea kura!!! lakini athari zake zilionekana kadri muda ulivyokuwa ukisonga. Kiwango cha uzazi kilishuka, na changamoto za kiuchumi ziliongezeka kutokana na idadi ndogo ya watu wanaofanya kazi. Serikali ya Korea Kusini sasa inajitahidi kuhamasisha ndoa, mahusiano, na uzazi ili kurekebisha hali hii, lakini ni vigumu kubadili mtindo huu ambao umepata nafasi kubwa kwenye jamii.

Nchini Ujerumani, changamoto zinazohusiana na uzazi pia zinajitokeza. Licha ya jitihada za serikali kutoa msaada wa kifedha kwa familia na likizo ya uzazi, kiwango cha uzazi kimeendelea kuwa cha chini, na hivyo kuathiri mfumo wa kijamii na kiuchumi. Ujerumani inategemea wahamiaji kuingiza nguvu kazi mpya ili kupunguza athari za upungufu wa watu.

HAPA NCHINI TANZANIA, kuna mwelekeo wa kijamii unaojitokeza, kama vile kauli ya “KATAA NDOA”, SINGLE MOTHERS, MASHANGAZI!!! inayosambaa kupitia mitandao ya kijamii na NYIMBO za wasanii. Ingawa inaweza kuonekana kama MZAHA au mtindo wa kupendeza, athari zake ni kubwa. Vijana wengi wanajikuta wakifuatilia mitindo hii, na baadhi yao wanaanza kuona ndoa na familia kama vitu visivyo muhimu. Wasanii kama The True Boy… wamechochea lifestyle hii kwa kutoa wimbo unaosema "Nakula Ujana", jambo linalowaathiri vijana na kuhamasisha hali ya kutokuthamini ndoa. Hii ni hatari, kwa sababu mabadiliko haya yanaweza kuathiri jamii kwa muda mrefu.

Ufaransa imekuwa ikijitahidi kurekebisha sheria zake kuhusu haki za wanawake, ikiwa ni pamoja na kuruhusu utoaji wa mimba ili kuhakikisha haki za wanawake zinaheshimiwa hili lilifanyika kisiasa na madhara yake yanaonekana. Nchini Marekani, viongozi kama Kamala Harris na chama chake cha Democratic wameendelea kuunga mkono haki za wanawake na ulinganifu wa jinsia, ikiwa ni pamoja na masuala ya ndoa za jinsia moja na haki ya kutoa mimba na madhara yake YANAONEKANA. Hata hivyo, watetezi wa sera za kihafidhina kama Donald Trump wamepingana na mwelekeo huu, wakiwa na maoni tofauti kuhusu haki za kikatiba na maadili ya jamii. kuna misemo maarufu kama CHILDLESS CAT LENGO KUHAMASISHA WANAWAKE KUTOKUZAA NA BLAA BLAA KIBAO

Kwa upande wa Korea Kusini, serikali imekuwa ikitumia mabilioni kuhamasisha ndoa na uzazi, lakini inakutana na changamoto kubwa kutokana na mabadiliko ya kimazingira na mtindo wa maisha wa vijana. Korea sasa imeamua kuachana na mitindo ya kijamii ya zamani na kuwekeza zaidi katika sera za kiuchumi na kijamii ili kurejesha misingi ya familia na ndoa, lakini kazi bado ni ngumu.

Madhara ya mabadiliko haya yanaweza kuonekana kama ni ya muda mfupi, lakini ni wazi kwamba yana athari kubwa kwa familia na jamii kwa ujumla. BASATA, kama chombo cha kusimamia maadili ya sanaa na utamaduni nchini TANZANIA, kinapaswa kuchukua jukumu kubwa katika kudhibiti na kuongoza mwelekeo wa kijamii, ili kuepuka madhara makubwa yatakayojitokeza kwa vizazi vijavyo. Hatuwezi kuruhusu kila kitu kutendeka kwa sababu tu watu wanadai uhuru au haki bila kujali athari zake kwa jamii nzima.

Tanzania inapaswa kuzingatia masuala haya kwa umakini. Wakati ni muhimu kuzingatia mabadiliko na maendeleo ya kijamii, ni lazima tuhifadhi maadili yetu na misingi ya familia. Kama ilivyokuwa kwa Urusi, Japan, na Korea Kusini, changamoto za kupungua kwa idadi ya watu na kuvurugika kwa familia ni hali inayohitaji mjadala wa kina na sera za busara. Tunapaswa kujifunza kutoka kwa mifano ya mataifa haya na kuhakikisha kuwa tunaendeleza mwelekeo wa kijamii utakaosaidia familia zetu kuendelea kuwa nguzo muhimu za jamii.

"Tuishi kwa heshima na maadili yetu, tutunze familia, na tuzingatie asili yetu ili tuendelee kuwa na jamii bora."
 

Attachments

  • CUT LADY.jpg
    CUT LADY.jpg
    47.1 KB · Views: 8
  • CAT LADY.jpg
    CAT LADY.jpg
    9.5 KB · Views: 7
  • CATLESS CHILD.jpg
    CATLESS CHILD.jpg
    5.6 KB · Views: 7
Back
Top Bottom