Katambi: Kuna mambo ya utekaji yanafanyika na raia wenyewe kwa uhasama na chuki

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Katika mahojiano na ayo TV, Waziri wa Mambo ya ndani, Patrobas Katambi, ameeleza kuwa matukio mengi ya utekaji na mauaji yanayoripotiwa nchini yanatokana na migogoro ya kibiashara, uhasama wa kijamii na uhalifu wa kawaida wa raia kwa raia, na si maelekezo ya mamlaka za serikali kama inavyovumishwa.

Katambi amesema kuwa serikali haina utaratibu wa kuteka bali inakamata wahalifu kwa mujibu wa sheria, huku akikiri kuwa matukio machache yanayohusisha watumishi wa umma hutokana na utashi au visa binafsi vya watu hao na tayari hatua kali za kisheria na kijeshi zimekuwa zikichukuliwa dhidi ya askari na maofisa wanaobainika kukiuka maadili.

Your browser is not able to display this video.
 
Polisi wafanye kazi. Habari za kufokea watu hamna. Huyu naye wasengerema kitambo.Raia wamefikia hatua ya kutekana na kuuana wewe ofisini unafanya nini sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…