Katavi: Ashikiliwa na Polisi kwa kupanga njama za mauaji ya Mchepuko wa Mkewe mdogo

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
JESHI la Polisi mkoani Katavi linamshikilia Machia Mbasa (65) kwa tuhuma za kudaiwa kulanjama za kujaribu kumuua Mabula Ntemange (37) huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Katavi Ali Makame Hamad, amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Lwafe wilayani Tanganyika mkoani humo, ambapo amesema mtuhumiwa amekua akimtuhumu Mabula kutoka kimapenzi na mke wake mdogo pia kuchukua kodi katika vibanda vyake vya biashara vilivyopo katika kitongoji cha Lwafe wakati yeye akiwa gereza la mahabusu Mpanda kwa tuhuma za mauaji.

Jeshi la Polisi baada ya kupokea taarifa hizo lilichukua hatua za haraka na kufanikiwa kuzima jaribio hilo kwa kumkamata mtuhumiwa.

Makame amesema mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alikiri kupanga njama ya kufanya hivyo huku akieleza aliwakodi wauaji wawili kutoka Kaliua mkoani Tabora na baada ya kufika Mpanda walipokelewa na mtuhumiwa nakisha kuwaficha maporini wakati wakisubili kutekeleza mauaji hayo.

Hata hivyo inadaiwa kuwa mtuhumiwa Mbasa amekua akituma ujumbe wa vitisho vya mauaji kwa njia ya simu kwa watu wengine wawili ambao ni Charles Lugembe na Dogani Malima wote wakazi wa kijiji cha Mwamkulu mkoani Katavi.

Kamanda amesema mtuhumiwa bado anaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao mzima wa watu anaoshirikiana nao kufanya mauaji na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Chanzo: Nipashe
 
Miaka 65 una mke mdogo, bado unakimbizana na penzi penzini.mpaka kupanga njama za mauwaji ...khaa jamani ,kwaiyo na utu uzima uwo bado anawivu wa mapenzi dunia simama kwanza...
 
JESHI la Polisi mkoani Katavi linamshikilia Machia Mbasa (65) kwa tuhuma za kudaiwa kulanjama za kujaribu kumuua Mabula Ntemange (37) huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Katavi Ali Makame Hamad, amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Lwafe wilayani Tanganyika mkoani humo, ambapo amesema mtuhumiwa amekua akimtuhumu Mabula kutoka kimapenzi na mke wake mdogo pia kuchukua kodi katika vibanda vyake vya biashara vilivyopo katika kitongoji cha Lwafe wakati yeye akiwa gereza la mahabusu Mpanda kwa tuhuma za mauaji.

Jeshi la Polisi baada ya kupokea taarifa hizo lilichukua hatua za haraka na kufanikiwa kuzima jaribio hilo kwa kumkamata mtuhumiwa.

Makame amesema mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alikiri kupanga njama ya kufanya hivyo huku akieleza aliwakodi wauaji wawili kutoka Kaliua mkoani Tabora na baada ya kufika Mpanda walipokelewa na mtuhumiwa nakisha kuwaficha maporini wakati wakisubili kutekeleza mauaji hayo.

Hata hivyo inadaiwa kuwa mtuhumiwa Mbasa amekua akituma ujumbe wa vitisho vya mauaji kwa njia ya simu kwa watu wengine wawili ambao ni Charles Lugembe na Dogani Malima wote wakazi wa kijiji cha Mwamkulu mkoani Katavi.

Kamanda amesema mtuhumiwa bado anaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao mzima wa watu anaoshirikiana nao kufanya mauaji na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Chanzo: Nipashe
Atubu kwa Mungu
 
Back
Top Bottom