Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi, Onesmo Buswelu amechukizwa na kitendo cha Mkandarasi kuchelewesha ukamilishaji wa ujenzi wa Barabara ya kutoka Mnyagala - Mwikang’ombe kwenda Kayenze yenye urefu wa Kilometa 9.86 ambapo imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa Wananchi wa ambao wanatumia Barabara hiyo kila siku.
Buswelu amemuagiza Mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi wa kalavati na kivuko cha muda kinachotumiwa na wananchi kuvuka kwenda upande wa pili, kisha kuendelea na ujenzi wa Barabara yote.