LGE2024 Katavi: Inadaiwa Rhoda Kunchela aitwa polisi kwa mahojiano. SACP Ngonyani asema kama kaitwa aitikie wito na si kukimbilia kwenye mitandao!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Screenshot_20241130_095603_Instagram.jpg

Inadaiwa kuwa Jeshi la Polisi mkoani Katavi kupitia kwa Mkuu wa Upelelezi mkoani humo limemuita kwa mahojiano Mwenyekiti wa CHADEMA wa mkoa wa Katavi Rhoda leo, Jumamosi Novemba 30.2024 asubuhi

Kwa mujibu wa Rhoda mwenyewe, amedai kuwa kupitia wito huo aliopatiwa Novemba 29.2024 ameambiwa kuwa Jeshi la Polisi linataka kumuhoji kuhusiana na tuhuma alizotoa Novemba 28. 2024 kwenye vyombo vya habari ambazo ndani yake kuna tuhuma za jinai kwa kuwa Jeshi hilo limeanzisha uchunguzi.

Kupata taarifa na matukio yote kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Baada ya kupata taarifa hiyo, Jambo TV imezungumza kwa njia ya simu mapema leo, Jumamosi Novemba 30. 2024 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani ambaye kwa maelezo yake hajathibitisha moja kwa moja kufahamu kuhusu uwepo wa taarifa hiyo.

Hata hivyo, Kamanda Ngonyani amehoji kama mtu huyo ameitwa Polisi kwa nini asiende kusikiliza wito huo badala yake anakimbilia mitandaoni, sambamba na hilo Kamanda huyo amemtaka mwandishi wa Jambo TV kufika ofisini kwake endapo anataka kupata undani wa suala hilo.

Tuhuma alizotoa Rhoda zipo kwenye video hii karibu na mwishoni: LGE2024 - Mwenyekiti CHADEMA Katavi: Mkishapiga kura nendeni kwa Mtendaji mwambieni ukipindua matokeo sisi tunapinduka na wewe!

"Sasa kama ameambiwa hivyo si atii sheria bila shuruti, kama amekuambia na kama wamemuita si atii sheria bila shuruti kama wamemuita, kama hajaitwa sawa lakini kama ameitwa atii sheria bila shuruti, mimi wewe ndio umeniambia, wewe ndio uliyeniuliza mwanahabari na nasema kama ameitwa atii sheria bila shuruti, sasa kama ameitwa ndio anakimbilia huko mitandaoni au kwenye vyombo vya habari?" -SACP Ngonyani
 
Mitandao ijue kuwa kaitwa......wanaweza kumpoteza milele....sifa kwa watawala
 
Ila CHADEMA itawasumbua Sana CCM . Pamoja na kujipa ushindi wa Asilimia 100 bado wanahangaika na CHADEMA. Na kumbuka mwaka 2020 waliposhinda ubunge viti vyote kasoro viwili walihangaika Tena kwenda kuwasaka akina Halima ndege wa CHADEMA.
 
Huyu naye hivi aliitwaga
 
Attachments

  • 5693904-733139b74b770431863bceb3e11f571f.mp4
    2.3 MB
Mchakato wa huyu mama Kamanda RPC kuwa hapo kwenye hiko kiti ulikuwajekuwaje hapo katikati😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom