Katavi: Madaktari Bingwa 18 kutoka Marekani kutua Hospitali ya Tanganyika

Katavi: Madaktari Bingwa 18 kutoka Marekani kutua Hospitali ya Tanganyika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi, Dkt. Alex Mrema amesema wanatarajia kupokea timu ya Madaktari Bingwa 18 kutoka Nchini Marekani kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu ya upasuaji ambapo itafanyika bila malipo (bure).

Madaktari hao wanatarajia kufika tarehe 06.04.2024 ambapo wanatarajia kutoa huduma kwa Wananchi wenye changamoto ya magonjwa yanayohitaji upasuaji.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanganyika, Juma Shabani amesema ujio wa madaktari hao utaleta tija na unafuu kwa Wananchi wenye magonjwa yanayohitaji upasuaji ambapo amewakaribisha Wananchi walio karibu na hospitali hiyo ikiwemo mikoa jirani kufika kuanzia tarehe 06.04.2024.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la The Norbert and Friends Mission (NFM-Bright), Joel Yalanda amesema wataendelea kushirikiana na serikali katika kuhudumia watanzania katika nyanja ya afya hasa wakijikita katika magonjwa yanayohitaji upasuaji.
 
Upasuaji wa makalio na dushe kama pale Mloganzila?
 
Back
Top Bottom