Pre GE2025 Katavi: Matukio Yanayojiri Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pre GE2025 Katavi: Matukio Yanayojiri Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Katavi ni 1,152,958; wanaume 569,902 na wanawake 583,056.

Mkoa wa Katavi una Halmashauri tano (5) na majimbo ya uchaguzi matano (5) ambapo Jimbo la Mpanda Vijijini linaongoza kwa kuwa na watu wengi (371,836) likifuatiwa na Jimbo la Mpanda Mjini (watu 245,764). Jimbo lenye idadi ndogo ya watu ni Katavi ambalo lina watu 118,818.
  • Mpanda Vijijini - Idadi ya watu: 371,836
  • Mpanda Mjini - Idadi ya watu: 245,764
  • Nsimbo - Idadi ya watu: 201,102
  • Kavuu - Idadi ya watu: 215,438
  • Katavi - Idadi ya watu: 118,618
Soma Pia: Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Katavi.jpg
Hali ya kisiasa
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, Mkoa wa Katavi ulijitokeza kama moja ya maeneo ambapo chama tawala, CCM, kilipata ushindi mkubwa na kudhibiti nafasi zote za ubunge kwa kura nyingi. Hali hii ilitofautiana na chaguzi za miaka iliyopita ambapo kulikuwa na ushindani wa kisiasa wa kiwango fulani, hasa kutoka kwa vyama vya upinzani kama CHADEMA na ACT Wazalendo.

Katika jimbo la Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi (CCM) alipata kura 24,020 dhidi ya Rhoda Kunchela wa CHADEMA aliyepata kura 13,611

Katika jimbo la Katavi/Mlele, Isack Aloyce Kamwelwe (CCM) alishinda bila kupingwa


JANUARI
  1. Pre GE2025 CHADEMA Katavi yasema inaunga mkono kauli ya Mbowe ya kuandamana Januari 24
  2. Pre GE2025 KATAVI: Wajumbe wa Mkutano mkuu CHADEMA Taifa watangaza kumuunga mkono Tundu Lissu
FEBRUARI - 0

MACHI
 
Back
Top Bottom