JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mgombea wa nafasi Mwenyekiti wa Kijiji cha Kabwaga, Kata ya Mwamkulu Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi, Helman Lutambi Mzee amesema Novemba 27, 2024 siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa amedai kupigwa na Diwani wa Kata hiyo, Kalipi Katani na kumsababishia maumivu makali mwilini mwake.
Ameeleza licha ya kuchukua hatua ya kwenda kutoa taarifa kwa polisi kata alijibiwa na polisi kata hayo kuwa hana uwezo wa kumsaidia kwa sababu zoezi hilo liko juu ya uwezo wake.
Mzee ametoa malalamiko hayo akisisitiza kuwa kitendo cha kupigwa kilikuwa na nia ovu ya kufifisha juhudi zake za kufanya ufuatiliaji wa haki na uwazi ili kudhibiti njama zozote za hujuma.
Pia, soma: LIVE - LGE2024 - Special Thread: Matukio ya Rafu za Uchaguzi na Malalamiko kwenye Zoezi zima Uchaguzi Serikali za Mitaa