JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
TAKUKURU mkoa wa Katavi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa, Agosti 24, 2022 imefungua shauri la jinai Na. CC. 95/2022 dhidi ya Elisha Christopher Mashamba ambaye ni muongoza watalii katika hifadhi ya misitu ya Tongwe East - Nkondwe Waterfalls Camp.
Ameshitakiwa kwa makosa ya kuomba na kushawishi rushwa ya sh. 50,000/=. Kesi hiyo imesikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mhe. Gway Sumaye na katika kesi hiyo mshtakiwa amekiri makosa yake na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya sh. 500,000/=, ambapo mshitakiwa ameomba kulipa faini na kupelekwa gerezani kwa maelekezo ya hakimu kuwa ndugu zake watakapoleta hiyo faini atatolewa gerezani.