Katavi: Muongoza watalii ahukumiwa miaka mitatu jela kwa kuomba rushwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
TAKUKURU mkoa wa Katavi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa, Agosti 24, 2022 imefungua shauri la jinai Na. CC. 95/2022 dhidi ya Elisha Christopher Mashamba ambaye ni muongoza watalii katika hifadhi ya misitu ya Tongwe East - Nkondwe Waterfalls Camp.

Ameshitakiwa kwa makosa ya kuomba na kushawishi rushwa ya sh. 50,000/=. Kesi hiyo imesikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mhe. Gway Sumaye na katika kesi hiyo mshtakiwa amekiri makosa yake na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya sh. 500,000/=, ambapo mshitakiwa ameomba kulipa faini na kupelekwa gerezani kwa maelekezo ya hakimu kuwa ndugu zake watakapoleta hiyo faini atatolewa gerezani.
 
Takukuru virushwa vidogovidogo mbona mnavikomalia
Ila zile za mabiliona,mamilion hazina nguvu

Ova
 
Sawa dagaa kanaswa ila nashauri wasisahau kufatilia mapapa wa sensa na ktk idara mbalimbali kuna mapapa huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…