Katavi: Mwanakijiji mbaroni kwa kukamatwa na meno ya tembo

Katavi: Mwanakijiji mbaroni kwa kukamatwa na meno ya tembo

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Mwanakijiji wa Kitongoji cha Ipota, Kijiji cha Ikuba, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi, Shija Ntumbili anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukamatwa na meno ya Tembo mawili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Ally Hamad Makame amewaambia Wandishi wa Habari kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa kufuatia msako makali uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Askari wa TANAPA.

Amesema kabla ya mtuhumiwa huyo kukamatwa Polisi walikuwa wamepata taarifa juu ya mtuhumiwa huyo kujihusisha na biashara haramu ya meno ya Tembo.

Baada ya kuwa wamepata taarifa hizo ndipo Polisi kwa kushirikiana na Askari wa TANAPA walianza kufanya msako mkali.

Kamanda Ally Hamad Makame ameeleza kuwa kufuatia msako huo ndipo walipofanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa ameyahifadhi meno hayo ya tembo mawili ndani ya nyumba yake.

Amebainisha kuwa taratibu zinaendelee za kwenye idara husika ili kuweza kujua meno hayo mawili yanathamani ya kiasi gani.

Amesema mtuhumiwa bado anaendelea kushikiliwa na anatarajiwa kufikishwa wakati wowote Mahakamani ili akajibu tuhuma zinazo mkabili.
 
KATAVI KUNA MACHIMBO YA DHAHABU!?? KUNA JAMAA YANGU ANANISHAWISHI NITAFUTE 10ML NIKABAHATISHE UKO.
 
Back
Top Bottom