Katavi: Wanaume wamewasusia wanawake kushiriki mazishi ya watoto kutokana na imani za kishirikina

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Hamjambo?

Wanaume wa kitongoji cha Namanyere kwenye mji mdogo wa Majimoto mkoa wa Katavi wamesusia wanawake kushiriki maziko ya watoto wanaofariki kwa madai kwamba vifo ni vya ushirikina unofanywa na wanawake.

===

Wanawake-kuzika62c74254bcdf-720x470.jpg

Kwa utamaduni wa maeneo mbalimbali nchini Tanzania, unapotokea msiba wanaume ndiyo huongoza mazishi kuanzia uchimbaji kaburi, hata ibada mbalimbali pale kaburini.

Hata kama wanawake wataenda makaburini, kwa baadhi ya imani ambazo zinaruhusu hawatahusika na uchimbaji kaburi, au uingiaji ndani kaburini kwenda kuzika iwe mtoto au mtu mzima, ingawa kwa baadhi ya maeneo machache watoto wachanga waliozaliwa na kufariki muda huohuo huwa wanawake wanazika.

Sasa iko hivi wanaume wanaoishi Kitongoji cha Namanyere, Kata ya Majimoto Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi wamesusia kufanya shughuli za mazishi ya watoto wanaofariki kwenye kitongoji hicho, kwa madai ya kukithiri kwa idadi ya vifo vya watoto, hivyo jukumu hilo la kuzika linafanywa na wanawake.

Hali hiyo sasa imezua sintofahamu, kwani haijawahi kutokea kwenye kitongoji hicho kwa shughuli za mazishi kufanywa na wanawake badala ya wanaume.

Akizungumza mkazi wa kitongoji hicho, John Madirisha, amesema wanaume wamesusia kufanya shughuli za mazishi kutokana kuongezeka idadi ya vifo vya watoto kuanzia umri wa kuzaliwa hadi miaka miwili.

Amesema idadi hiyo ya vifo imekuwa kubwa na kuanza kuwatia hofu juu ya vifo hivyo na kuamini vinatokana na nguvu ya giza.

‘’Sisi tumechoka kuzika kila siku watoto wanakufa na hao wanaowaua ni baadhi ya wanawake wa kitongoji hiki kwa kisingizio cha surua, wazike wenyewe,’’ amesema Madirisha.

Naye Michael Masanja mkazi wa kitongoji hicho, ameeleza kuwa idadi ya vifo imekuwa ni kubwa kwenye kitongoji hicho, kwani watoto wanaofariki kwa wiki ni kati ya wanne hadi watano.

Amedai kuwa hapo nyuma kulikuwa na mlipuko wa ugonjwa wa surua, lakini hadi sasa bado vifo vimeendelea, hali inayofanya kutokubaliana na vifo hivyo, kwani wanaamini kuna ushirikina unaoendelea kufanywa na baadhi ya wanawake kwenye kitongoji hicho kwa kisingizio cha ugonjwa wa surua.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Namanyere, Teresia Wikula amekiri kuwa ni kweli wanaume wa kitongoji hicho wamesusia kufanya shughuli za mazishi na shughuli hizo kwa sasa zinafanywa na wanawake.

Amebainisha kuwa kwa wiki wamekuwa wakizika watoto wanne mpaka watoto watano, hali ambayo haijawahi kutokea katika kitongoji hicho.

Hata hivyo amesema vifo hivyo ni kutokana na ugonjwa wa surua na sio ushirikina kama wanavyodhani wanaume wa eneo hilo.

Amesema maofisa wa afya wamekuwa wakifika kitongojini hapo na kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kutoa chanjo, lakini mwitikio wa wananchi hao umekuwa mdogo.

Habari Leo
 
Waamini ushirikina ni watu wapumbavu kabisa dunia hii. Wabantu tulichelewa kuendelea sababu ya hili. Serikali ifanye kupeleka wataalamu wa afya ya jamii wakaangalie nini chanzo cha vifo vya watoto. Na hao wapumbavu wapewe elimu na kama inawezekana na kichapo wapewe akili zikae sawa.
 
Acha kuropoka ,Arusha Kuna kilombero ,kwani hujui Kilombero Iko Morogoro?

Huo ni mtaa wa Namanyere uliopo Majimoto,mlele Katavi hamaanishi hiyo wilaya
Nitolee upumbavu wako kwani unashindwa nini kutoa ufafanuzi mpaka uongee kama unaharisha,Idiot huwezi ukamsahihisha mtu kwa lugha nzuri mpaka uropokwe hivyo?jifunze kuwa na lugha ya staha especially unapokuwa kwa watu waliostaarabika,
 
Wapimbwe wavaa sketi wanaamini sana hayo mambo halafu namanyere ipo sumbawanga sio majimoto umbali kutoka majimoto hadi namanyere ni zaidi ya km 185
Mimi ni mwandishi wa Mazingira nimefika Majimoto kuna kitongoji kinaitwa Namanyere, achana na Namanyere Mji mkuu wa wilaya ya Nkasi, hapo paliitwa Namanyere sababu waanzilishi wa kitongoji hicho wengi walihamia toka Namanyere.
 
Hamjambo?

Wanaume wa kitongoji cha Namanyere kwenye mji mdogo wa Majimoto mkoa wa Katavi wamesusia wanawake kushiriki maziko ya watoto wanaofariki kwa madai kwamba vifo ni vya ushirikina unofanywa na wanawake.

===

View attachment 2518997

Kwa utamaduni wa maeneo mbalimbali nchini Tanzania, unapotokea msiba wanaume ndiyo huongoza mazishi kuanzia uchimbaji kaburi, hata ibada mbalimbali pale kaburini.

Hata kama wanawake wataenda makaburini, kwa baadhi ya imani ambazo zinaruhusu hawatahusika na uchimbaji kaburi, au uingiaji ndani kaburini kwenda kuzika iwe mtoto au mtu mzima, ingawa kwa baadhi ya maeneo machache watoto wachanga waliozaliwa na kufariki muda huohuo huwa wanawake wanazika.

Sasa iko hivi wanaume wanaoishi Kitongoji cha Namanyere, Kata ya Majimoto Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi wamesusia kufanya shughuli za mazishi ya watoto wanaofariki kwenye kitongoji hicho, kwa madai ya kukithiri kwa idadi ya vifo vya watoto, hivyo jukumu hilo la kuzika linafanywa na wanawake.

Hali hiyo sasa imezua sintofahamu, kwani haijawahi kutokea kwenye kitongoji hicho kwa shughuli za mazishi kufanywa na wanawake badala ya wanaume.

Akizungumza mkazi wa kitongoji hicho, John Madirisha, amesema wanaume wamesusia kufanya shughuli za mazishi kutokana kuongezeka idadi ya vifo vya watoto kuanzia umri wa kuzaliwa hadi miaka miwili.

Amesema idadi hiyo ya vifo imekuwa kubwa na kuanza kuwatia hofu juu ya vifo hivyo na kuamini vinatokana na nguvu ya giza.

‘’Sisi tumechoka kuzika kila siku watoto wanakufa na hao wanaowaua ni baadhi ya wanawake wa kitongoji hiki kwa kisingizio cha surua, wazike wenyewe,’’ amesema Madirisha.

Naye Michael Masanja mkazi wa kitongoji hicho, ameeleza kuwa idadi ya vifo imekuwa ni kubwa kwenye kitongoji hicho, kwani watoto wanaofariki kwa wiki ni kati ya wanne hadi watano.

Amedai kuwa hapo nyuma kulikuwa na mlipuko wa ugonjwa wa surua, lakini hadi sasa bado vifo vimeendelea, hali inayofanya kutokubaliana na vifo hivyo, kwani wanaamini kuna ushirikina unaoendelea kufanywa na baadhi ya wanawake kwenye kitongoji hicho kwa kisingizio cha ugonjwa wa surua.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Namanyere, Teresia Wikula amekiri kuwa ni kweli wanaume wa kitongoji hicho wamesusia kufanya shughuli za mazishi na shughuli hizo kwa sasa zinafanywa na wanawake.

Amebainisha kuwa kwa wiki wamekuwa wakizika watoto wanne mpaka watoto watano, hali ambayo haijawahi kutokea katika kitongoji hicho.

Hata hivyo amesema vifo hivyo ni kutokana na ugonjwa wa surua na sio ushirikina kama wanavyodhani wanaume wa eneo hilo.

Amesema maofisa wa afya wamekuwa wakifika kitongojini hapo na kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kutoa chanjo, lakini mwitikio wa wananchi hao umekuwa mdogo.

Habari Leo
@UMUGHAKA njoo utoe ushuhuda wa namanyere huku
 
Naalafu anatokea mlevi mmoja utasikia "watu wa pwani washirikina sana bwana"wakati matukio ya kichwa yanaongoza kanda ya kaskazini huko😁
Kanda ya kaskazini tena? we una chuki zako binafsi, watu wanaongelea habari za Katavi, Katavi iko kaskazini?
 
Back
Top Bottom