Katavi: Watu 15 wakamatwa kwa kumuozesha mwanafunzi kwa ng'ombe 12

Katavi: Watu 15 wakamatwa kwa kumuozesha mwanafunzi kwa ng'ombe 12

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Jeshi la polisi mkoa wa katavi limewakamata watuhumiwa 15 wakiwemo wazazi wawili kwa kumwozesha mwananfunzi wa darasa la tano anayesoma shule ya msingi ya Kaseke iliyopo manispaa ya Mpanda kwa mahari ya ngombe 12.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga amesema katika mohojiano na watuhumiwa hao jeshi liliweza kungundua mbinu ya udanganyifu waliyoitumia kwa kuwaweka wahusika wawili, Stela Paul na Samsoni Charles kama wanandoa.

Kamanda Kuzaga amesema jeshi la polisi lilifanikisha kuisambaratisha ndoa hiyo ya kimila huku likiendelea na juhudi ya kumtafuta muoaji aliyetoroka .

Aidha kamanda kuzaga amesema jeshi halitosita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu au kikindi cha watu na kuwafikisha Mahakamani.
 
Kuna baadhi ya watu shida zinawakwepa, wao wanazitafuta wenyewe. Wamepata walichotaka
 
Hivi,ukishamuoa huyo binti, unaenda kukasubiri kapanuke au huwa wananakachakaza hivyohivyo. Watu wakatili sana aisee.
 
Back
Top Bottom