Katazo jipya la zuio la matumizi la vifungashio vya plastiki laanza kutekelezwa

Katazo jipya la zuio la matumizi la vifungashio vya plastiki laanza kutekelezwa

Joined
Apr 9, 2022
Posts
66
Reaction score
32
Itambulike kuwa Nchi ya Tanzania ni miongoni mwa Nchi katika ukanda wa Afrika Mashariki ambayo limefuata nyayo za Kenya na Rwanda, kuweka katazo la matumizi ya Mifuko ya plastiki na amri hiyo ilisha anza kutekelezwa kwa mujibu wa makubaliano ya kimataifa ya kulinda mazingira dhidi ya bidhaa za plastiki.

Hayo yote yamejili baada ya Katibu Mkuu wa umoja wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam (SHIUMA) kukili kupokea katazo jipya kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, linalotaka kuzuia utumiaji vibebeo vya aina zote za plastiki(carrier bags).

Akizungumza na Mwakilishi wa Jamii Forum Issa amesema hatua kubwa na muhimu inaanza wakati muafaka.

"Tumejipanga kutekeleza agizo la Serikali lilipangwa kuanza kutekelezwa na tayari limeanza kutekelezwa jumatatu hii" alisema Issa.

Katikati ya wiki iliyopita Mkuu wa Mkoa Amos Makala alikutana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC) na kutoa katazo hilo ambalo alisema kumekuwepo na wimbi kubwa la matumizi ya mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku.

Katazo hilo kwa Tanzania lilianza kutumika, Juni, moja 2019 kwa kusudi la kuzuia athari za mifuko ya plastiki ni pamoja na kutunza Mazingira.

Kwani inakadiriwa kudumu hadi zaidi ya miaka 500 na hivyo kuleta athari za muda mrefu; uchafuzi wa Mazingira hasa kwa mifuko hii kuzagaa ovyo katika Mazingira.

Eidha changoto ya kuziba kwa miundo mbinu ya maji taka na mifereji kunaweza sababisha mafuriko, kuharibu mfumo wa ikolojia, bioanuai, vifo vya mifugo na wanyama wengine hususani mifugo na viumbe wa baharini wanapokula na kumeza mifuko hii.
 
vile vifuko mnavyowekea mihogo mtaani kwenu ni vya ngozi au?
 
Back
Top Bottom