Katazo la Bodaboda na Bajaji Dsm litakuja na pointi 3 za mezani

believer

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2012
Posts
639
Reaction score
216
Kuna wakati Godbless Lema aliwqhi kusikika akisema kazi ya Bodaboda sio kazi, kaul8 hii ilinitafakarisha sana, kwanza nilijaribu kuingia kwenye mawazo yake ili kuhukumu kwa haki. Ikumbukwe kuwa katika Jamii mtu anaweza kukushauri sio kwa jinsi inavyopaswa bali kwa jinsi yeye anavyoliona, na jinsi mtu anavyoliona jambo ni kutokana na uzoefu wake, exposure yake, ujuzi wake, utu wake, upendo wake na ujasiri wake. Baada ya kuyazingatia hayo nikathibitisha kuwa Lema anaweza alikua sahihi lakini watu wakachaguq kutoelewa, wakaaminishwa wasielewe nk nk.

Sasa kwanini tuko hapa tulipo, Wimborne mkubwa na ulio mkuu katika jamii ni vijana wajiajiri vijana wajiari,unategemea kwamba Wimborne kama huo ungeambatana na mawekezo ktk kutengeneza Fursa za makusudi mf badala ya Serikali kusema wanatoa mikopo kwa vijana waunde vikundi wapate mikopo, kumbe tungewekeza kwa vijana wenye Wazo/ Mawazo, wazo 1 linaweza kubeba vijana 300, ukipata vijana wenye mawazo 100, unaweza ukaguwa watu 30,000 ambao wana wategemezi nyuma ya wastani wa watu 5 kila 1,do the Maths.

Hakuna mtu anapanga kuwa Bodaboda is ipo isipokuwa hali ya uchumi na wimbo tunaoimbiwa kila siku tujiajiri ndio unatufikisha hapa. Lakini la muhimu pia ni ukweli wateja na jamii wanategemea sanausafiri wa Bodaboda na Bajaji. Kwahiyo ukirudi tena upande wa pili kwanini Jamii kwa ukumbwa wake inategemea sana usafiri huo, hiyo mada nyingine.

Kwakua usafiri huu unagusa hisia na sehemu kubwa ya Jamii, Bodaboda na Bajaji wamekuwa wakifanya kazi zao kwa uhuru, na pindi wanapokua wanahitajika kwaajili ya mikusanyiko na hamasa mbalimbali kwakweli hawako nyuma.

Ikiwa hivyo ndivyo nini kinatokea, wajibu wao umetengeneza haki, kama wanatumika nao wanajitumia,imekua Ajira, imekua mkombozi kwao lakini kwa jamii pia ktk suala zima la usafiri.

Sasa basi, sasahivi kuna katazo Jijini Dsm la Bodaboda na Bajaji kuingia ktkt ya Mji, na ufuatiliaji umeanza, ni jambo jema kwasababu naamini mamlaka haziwezi kuja na katazo lisilo na mantiki. Kinachonifikirisha mimi ni Je Jamii inayotegemea usafiri huu itakuaje, watoa huduma hawa ambao walishaaminishwa inakuaje mustakabari wa mabadiliko hayo kwenye vipato, mikopo, huduma kwa familia ,tukumbuke tulishawaambia hiyo ni Ajira na watoe huduma kokote tena washiriki na ulinzi shirikishi.

Hapa ndio narudi kwenye kichwa cha habari cha uzi huu, au ni ushindi wa meaning unaandaliwa, katazo linatoka, amsha amsha inatokea ya kamata kamata, halafu anajitokeza mkombozi 1 na kutoa tamko Bodaboda na Bajaji ni ndugu zetu , watu wetu waachweee watoe huduma kwa uhuru iwe katikati au kwenye kona ya Mji wasisumbuliwe. Watu wanapokea mkombozi anachukua pointi 3, halafu sasa itabidi mahali mahali au ikifika nyakati nyakati inabidi nao walipe fadhila, hasa kwenye hamasa nk nk nk nk. Linatatwa tatizo linaletwa halafu unaletwa ufumbuzi watu wanasepa na kijiji pointi 3 kwapani....till next time, ooh.
 
Tanzania nchi ya ajabu sana yaani kuna ujinga wa viongozi kushindwa kusimamia sheria zilizopo yaani bodaboda, machinga na bajaji ni janga kubwa sana kwanini inashindikana kuwaondoa.
 
Umeshawahi kuandika kitu humu JF kabla?
 
Boda boda ni kazi ndio maana wenzetu wakaona fursa na kuweka system nzuri, kuanzisha makampuni makubwa kama Uber
...
kuondoa tatizo moja(bodaboda/machinga) kunaibua tatizo lingine ukosefu ajira,uhaba wa usafiri nafuu na wa haraka
 
Anamaanisha, bodaboda zitapigwa marufuku halafu bodaboda na watu wengine watalalamika. Anatokea mwanasiasa mmoja anatoa amri bodaboda waachwe wafanye kazi. Mwanasiasa huyu ataonekana ni mkombozi na anajali wananchi. Hapo anajizolea ushindi point tatu mezani. Tengeneza tatizo halafu litatue.
 
Nika vaa na miwani lakini bado....Ni muda sasa kwa Jamii Forum kuweka, Voice record, itasaidia..
 
Hizi shule tulizoenda kusomea ujinga, ni taabu kweli kweli.....🚮
 
Mkutano wao wa nishati ukiisha watawarudisha mjini

Ova
 
Kwahiyo watu waanze kukaa maswaa mawili kwenye foleni kwenda mjini? Na mtu anawahi kikao.., no way, where there is DEMAND there is a WAY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…