Mwenendo wa taasisi za serikali na hata sekta binafsi zinavyokataza wananchi kupiga picha ama kuchukua video maeneo yenye kasoro ama kurekodi utendaji wa watumishi wa umma usio endana na maadili , lengo hasa la katazo hili huwa nini?
Unaweza ukaenda kwa mfano, muhimbili utakutana kabisa na mabango huruhusiwi kupiga picha. Sasa mtu unajiuliza niko na mgonjwa wangu siruhusiwi hata kupiga picha nae kama kumbukumbu wengine hawabahatiki kuondoka na wagonjwa wao pale sasa jamani hata picha za kumbukumbu huwezi piga. Huu usiri hadi lini?
Ukikaa ukifikiria ki undani utaona kwamba kwa sasa maboresho mengi yameweza kufanyika kwakua tu jamii iliweza kuibua matatizo mbalimbali kwa kutumia mitandao ya jamii. Sasa kuwakataza wananchi wasipige picha ama video ni kuonyesha dhahiri kuwa kuna jitihada zinafanywa ili jamii isijue hali halisi ya taasisi hizo.