Tractor zote ni nzuri shida inakuja kwenye vitu vifuatavyo:-
Location: wewe unataka uitumie eneo gani tanzania hii kwa mfano unaishi maeneo yenye ardhi ngumu sana unahitaji tractor yenye nguvu yaani 4WD. Kampuni nzuri ni SONALIKA, MAHINDRA, MASSEY, SWARAJ (Kwa maeneo yenye ardhi ngumu sana)
Kwa maeneo yenye ardhi laini na hutaki kulimia sana watu hata MASSEY FERGUSON 135 inatosha kabisa, cheap na lita 20 inaweza wa kulima hekari hadi kumi.
UPATIKANAJI WA SPEAR: Hapa ndo kwenye shida makampuni ya sasa yamebase kwenye utengenezaji wa tractor zenye nguvu ila spear ndo hamna ukiharibu kitu kidogo tu unaweza ukakaa mwaka mzima bila kufanya kazi hii ni kwa matrekta yote ya kisasa isipokuwa MASSEY FERGUSON KAMPUNI KONGWE YENYE SPEAR NYINGI nina ushuhuda sana katika hili.
PSYCHOLOGY YA CONSUMER: Siku hizi watu wanataka tractor zinazotembea sana wakati wa kulima so hilo nalo la kuzingatia sana kumbuka kiendacho kasi hushuka kwa kasi Massey ni Powerful but not faster kwenye ardhi ngumu sana. So nenda kisasa zaidi.
Asanteni
Zingatia USED ZIPO NA ZINATENGENEZEKA KWA KUANZIA SIO MPK UPATE MILLIONI 60 kwa ajili ya kumiliki Tractor Yako.