Mkuu....Rosa ni mrembo aisee halafu mdada mmoja mtu wa kazi kazi
Yupo pale kimkakati, unafikiri utatoa pesa kizembezembe? Lazima wakuwekee vilainishi.
Kuna siku nimeenda pale, kwanza nilipewa namba kumbe ni za ofisi ya Arusha. Sasa nashangaa nimepita Morocco, naona bango lao, nikasema hamad, acha nisogee karibu.
Lwanza ile ofisi ilivyo classic na wale wahudum nikasema leo nimekamatika, nikaelezea shida yangu nikapewa mtu akakague sasa...dah. Nikaambiwa 2.2 M kuweka seat cover ya kausafiri kangu wakati hapo tu inakaribia bei niliyonunulia.
Uzuri kulikua na sikukuu zinafuatia nikapata kisingizio sitakua na muda kwa sababu walisema watahitaji niiache chombo cha usafiri hapo kwa siku takriban nne.
Nikapata kuondoka huku nikiwa nakemea pepo mchafu kwa sababu nilikya kadri nnavyoongeleshwa, nazidi kukaa mkao wa kukubali kuiacha gari.
Nikasema wanawake wanamoyo sana, imagine kwa siku anakutana na ndoana ngapi na bado anazipangua zote?
Nikaambiwa niandike mawasiliano, hapo ndio nikachukua point tatu mezani bila jasho, kuna boss wangu mmoja alienda hapo kuna kitu niliandika pale wakakumbuka, kuniuliza nikasema nakielewa na huyo mtu tuko wote. Gafla graph ikapanda ikaonekana nimetingwa na kazi tu kumbe kichwani 2.2 M inazunguka...