masmo yenye prac yanakufanya uwe na kozi nyingi by the way zote ukjtahidi hamna ugumu wa kutisha me nasomea bios and chem kusoma ndo kla kitu sina sup wala carry.
Wale wanaosomesha vyuoni sio walimu, some time sisi tunakua tunashindwa kujipanga kimaisha, kuna rafiki yangu mmoja ni mwalimu tena Wa secondary O level na maisha yanaenda uzuri tu, yaani asubuhi anaingia kazini na akitoka mchana anapiga kazi Zake nyengine, tena mwenyewe anakwambia hakuna kazi nzuri kama ualimu
Ugumu au wepesi inategemea kujituma kwako kusoma, mapenzi kwa somo nk. Mimi nilisoma Physics, Chemistry na Biology. Kwangu somo gumu lilikuwa Organic Chemistry, lakini baadhi ya wanafunzi darasani waliona hilo ndio jepesi kuliko yote.
Angalia wewe una fall in love na masomo gani, na yepi ulikuwa unafanya vizuri huko madarasa ya nyuma
umasikini ni akili ya mtu, kama hii ya kwako.ni waalimu wangapi wana maisha mazuri kama madaktari na mainjinia? ni namna ya kufikiri ndo kinachotutofautisha.
fikiria hili, kozi ya edu ni miaka 3, mwalimu anaanza na mshahara wa 589000, na hupanda
hadi laki 7 na zaidi baada ya miaka 3. mda huo kwa mwenye akili huwa ameshafanya investment za kutosha, kozi ya udaktari ni miaka 5 na 1 wa mazoezi, akiingia kazini huanza na laki 9, je tofauti kubwa ya kimaisha kati ya watu hawa iko wapi kwa mantiki ya mshahara?
kwa muulizaji, soma kile unachopenda toka moyoni, ndo kitakachokuwa rahisi kwako kwani ndo kipawa kilichoumbwa ndani yako, na kupaliliwa na mazingira uliyokulia.