ndandambuli
JF-Expert Member
- Jul 2, 2017
- 948
- 641
Mke ambaye aliolewa na mume ambaye tayari alishakuwa na nyumba ya kuishi,ameishi na mumewe miaka mitatu baadaye anaamua kuondoka nyumbani kwa hiari yake mwenyewe ni baada ya kufumaniwa.
Mume anaamua kuoa mke mwingine maisha yanaendelea,miaka mitatu baadaye mume anafariki dunia ,huyu mke aliyeondoka baada ya kufumaniwa anaanza kudai nyumba iuzwe wagawane na mke mwenzie kwakuwa yeye ndiye alikuwa mke wa kwanza wa mume wao,na hakuachana na mumewe lla walitengana tu kwasababu fumanizi lilitokea.
Huyu mke wa pili anasema nyumba ni yake na mtoto wake kwasababu wakati anaolewa hakumkuta huyo bi mkubwa.
Je nani mwenye haki hapo ? na huyu bi mkubwa hakubahatika mtoto,bi mdogo ana mtoto mmoja.

Kituchakujiuliza, mke wakwanza walifunga ndoa? Na cheti cha ndoa kipo? Maana sheria ya ndoa hairuhusu kufungwa kwa ndoa nyingine kwa MTU ambaye yupo ktk ndoa inayoendelea. Hivyo kama bi mkubwa alifunga ndoa inayokidhi vigezo vyakisheria basi hio yapili si ndoa( NB; Hii nikwawale wakristo).
Lakini ikiwa waliishi pasi kufunga ndoa basi dhana ya ndoa itambeba huyo mwanamke wa pili.
Nakuhusu kuuza nyumba ya marehemu hilo niswala la mirathi, familia inapaswa kukaa na kuteua msimamizi wa mirathi ambae atapewa utaratibu na familia na baadae kuidhinishwa na mahakama. Na sihivyo huyo bi mkubwa anavyotaka kufanya.