Kati ya kiwanja na ng'ombe kipi kina maslahi zaidi?

Ukwel mtupu

Member
Joined
Jan 30, 2014
Posts
40
Reaction score
8
Wakuu mim nipo mwanza town na kama mjuavyo jiji la Mwanza ni kati ya majiji yanayokuwa kwa kasi sana nchini hivyo demand ya ardhi ni kubwa mno hali inayopelekea viwanja kupanda bei kila siku.

Binafsi nina kama sh laki nane cash ninataka ninunue eneo pembezon mwa mji lakin pia kuna mtu amenishauri ninunue ng'ombe kama wanne kwa bei ya lak 2@ halafu niwafuge kwa muda mchache then niwauze kwa bei ya juu halafu ndo ninunue eneo, sasa nashindwa kuelewa which is profitable?

Naombeni ushauri wakuu!
 
N'gombe mpaka uje kuwauza utahitaji uwe umewagharamia matunzo kiujumla, i.e: Chakula, madawa wakiugua, shelter n.k....

Kiwanja hakina gharama za matunzo. Hivyo basi nakushauri uchambue pro and cons za hiyo miradi miwili na ukadirie return yake itachukua muda gani kuipata kisha ufanye maamuzi.
 
Labda kwa kuongeza maelezo,unahitaji ubora kwenye nin,kama ni N'gombe hufa kiwanja akifi,
n'gombe atahitaji matunzo kama mkuu alivyokwisha kukwambia,kiwanja akihitaj vyote hivyo,
n'gombe ni asert ambyo thaman yake haipandi kwa kas kama ardhi
 
Chukua kiwanja kwanza kama hujawahi fanya biashara yo yote.
 
Chukua kiwanja mkuu halafu utaniuzia mimi baada ya miezi 3
 
Ikiwa kumbukumbu zangu zimekaa sawa 800,000 ni ngumu kupata kiwanja maeneo jirani na barabara kuu...Mabuki to Mkolani au Nyanguge to Kisesa.


Labda ndani huko vijijini maeneo ya Fela, Kona n.k

Yaweza kuwa alokwambia ununue ng'ombe ni kwa vile alitambua laki 8 haijai kulipia kiwanja cha maana.

Namjua dogo mmoja anafanya biashara ya kununua ng'ombe anakaa nao mwezi mmoja au miwili (wanakula mashudu sana) kisha anauza mara mbili ya bei.
Ila kama 800,000 ndio nyuzi 360 zako, usijaribu biashara ya ngo'mbe!!
 
Taja kabila kwanza vitu ukifanya vinaendana na kabila tujuzane kwanza
 
Mpaka muda wa kuwauza hao ng'ombe, viwanja vitakuwa vishapanda bei.. na mwisho wa siku faida yote uliyoitengeneza ikawa haina maana...

By the way, ushawaza hao ng'ombe wakifa inakuwaje?

 
Unauliza kabila lake, kwani kasema anataka kutambika? ( JKN) !!!!!!!

Asanten sana wakuu kwa ushauri wenu sasa naamin ntafanya best choice, kuna mkuu kaniuliza kuhusu kabila langu mim ni mchaga wa marangu kabisa!!!
 
Nunua shamba,
baada ya mwaka utapata zaidi ya mara kumi ya initial cost
lakini ng'ombe ni probability alafu wanahitaji matunzo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…