Kati ya kutunza Fedha zako Benki kama Akiba yako ya baadae au Uwekeze katika Ardhi (Kununua tu Viwanja) ipi ni Mkombozi Kwako kwa baadae Maishani?

Real estate bongo ni biashara isiyo na faida.

Kama una hela weka fixed deposit ama akaunti ya amana. Utaishi bila stress na presha huku ukila pesa zako taratibu..

Nakupa mfano. Ukanunua kiwanja eneo zuri mfano hapa Dar kama Goba, Salasala ama Madale. Kujenga apartment 1 yenye room 4 na sebule 2, yaani 2 in one kwa bei ya chini kabisa ni 70m.

Tukadirie kiwanja kina ukubwa wa Sq 1000. Hapo utajenga nyumba 3 zenye apartment jumla 6.

Bei ya kiwanja ni 70m, nyumba 3 zenye apartment 6 ni 210 jumla 280.

Apartment 1 bei ni 600k kwa mwezi, kwa mwaka ni 7.2. apartment ziko 6 kwa mwaka unapata 43.2m. Hivyo kurudisha pesa yako(initial investment ya 280m) utahitaji miaka 7 kwa wastani.

Hapo miaka 7 tumekadiria miaka yote iko full rented ama occupancy rate ni 100%. Maana yake occupancy rate ikipungua hata kwa 20% kwa kipindi chote hicho pay back period inaongezeka kwenda miaka 8 hadi 9.

Hapo tumefanya wewe baba mwenye nyumba huna gharama nyingine za matengenezo wala ukarabati. Ukiweka hizo gharama maana yake pay back period inaongezeka hadi 10+.

Turudi bank. Ukiweka 280m bank leo ukapata deposit rate ya 12% fixed kwa miaka 8. Kwa mwaka utapata interest ya 33.6m. tuchukulie interest itakua kwenye original investment ya 280m kwa miaka 8 utapata 270m jumlisha na 280m ya awali utakua na 550m bank.

Tuje scenario 2, ile 33.6m inaongeza balance kila mwaka na interest rate iko charged on balance(maana yake no withdrawal) kwa maan akwmaba ni compounding interest kwa miaka 8 utapata interest ya karibu 350 na original investment yako unakua na 630+m

Jiulize, baada ya miaka 8 ile investment yako ya kwanza baada ya pay back period itakupa 150% ya original investment kwenye real estate ?Jibu ni hapana.

Weka pesa bank ule maisha kwa raha mustarehe.
 
Ni bank gani inayotoa rate ya 12% kwa Mwaka kwa initial depot ya 280m?
 
Ni bank gani inayotoa rate ya 12% kwa Mwaka kwa initial depot ya 280m?
Mkuu unayo hiyo hela nenda bank wanatoa hiyo riba.

Factors zinazo determine deposit rate ya kwanza ni amount na ya pili ni time. Ukiwa na hiyo hela bank wanakaribisha majadiliano vizuri tu.

Nakupa mfano. Kama 1 year Treasury Bills rate ni 11.5656(March 27, 2024) unadhani bank ili wakuvutie wewe uwape deposit watakupatia ngapi? Obvious watakupatia kuanzia 12.
 
Vipi kuhusu inflation? Elfu 10 ya 2020 ilikua inanunua vitu vingi kuliko ya sasa hvi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…