Kwahiyo unataka kusema kiama cha Gray Mgonja/Vicent Mrisho kimefika? kwa vyovyote kama kuna mtu wa kupanda kizimbani basi ni Gray Mgonja na hii inaweza kuhusu matumizi mabaya ya madaraka! hata kama hakuna atakayefungwa katika kesi ya Yona/Mramba na pengine hata Mgonja lakini itaset precedent kwamba ukiwa mtumishi wa umma lazima utumie nafasi hiyo kwa maslahi ya umma na si kwa maslahi ya tumbo lako binafsi na familia yako.