Ni vyema tukajiuliza na sehemu nyingine pia kama kwetu udini unatangulia kabla ya utaifa, uzalendo, uadilifu na uchapa kazi?? Tujiulize na maswali kama haya:
Na katika viongozi wakuu wa kitaifa, waislam ni wangapi na wakristo ni wangapi? Na katika mawaziri waislam ni wangapi na wakristo ni wangapi? Na katika wabunge waislamu ni wangapi na wakristo ni wangapi? Katika wakurugenzi waislamu ni wangapi na wakristo ni wangapi??? Na katika madereva hiace/dcm/costa/mabus ya mikoani waislamu ni wangapi na wakristo ni wangapi??? Katika daladala uliyopanda leo kwenda kazini kwako waislamu walikuwa wangapi na wakristo wangapi?? Na katika wenye magorofa pale kariakoo/posta/etc waislam ni wangapi na wakristo ni wangapi?? Etc.. etc..etc. The list can grow very big.
Haya yote yanaonyesha taifa letu halina nguzo za kitaifa, ndo maana watu kama redio zenye leseni yenye masharti wazi kabisa inaweza kuanzisha mjadala kama huo, na viongozi wa nchi wakiwemo waliotoa hizo leseni wakakaa kimya.
Tukitaka kuibomoa nchi hii tuendeleze udini, na tuziachie radio kama hizo ziendeleze hiyo mijadala