Kati ya maji ya kunywa ya uvuguvugu, na maji ya kunywa ya kawaida, yapi yana nguvu zaidi kitiba?

Kati ya maji ya kunywa ya uvuguvugu, na maji ya kunywa ya kawaida, yapi yana nguvu zaidi kitiba?

kufanakupona

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2015
Posts
522
Reaction score
421
Wakuu nimejiuliza nimekosa majibu, kwa sababu hapa JF kuna vichwa vya aina mbalimbali, natumai nitapata majibu na ufafanuzi mzuri.

1: Anayekunywa maji ya uvuguvugu alfajiri, na anayekunywa maji ya kawaida alfajiri, nani ananufaika zaidi?

2: Ya uvuguvugu na ya kawaida, yapi yana mechanism nzuri mwilini?

3: Taja njia yoyote isiyo na madhara kwa afya ya binadamu ya kuhifadhi maji ya uvuguvugu yawe ya uvuguvugu muda wote.
 
Yote sawa kazi ya maji ni moja kwa aina zote
Maji ya uvuguvugu na ya kawaida hayawezi kuwa sawa ki-mechanism hata siku moja. Kwahiyo hapo lazima kutakuwa na yapi ni zaidi kuliko mwenziye.
 
Mi huwa napiga ya uvuguvugu na ya kawaida kama lita 6 kwa siku na mambo yanaenda poa tu
 
Mi huwa napiga ya uvuguvugu na ya kawaida kama lita 6 kwa siku na mambo yanaenda poa tu
Ukipiga mara ya uvuguvugu, mara ya kawaida, huoni kama unachanganya madawa?
Unavyoona wewe, ya uvuguvugu na ya kawaida, yapi yana nguvu zaidi kitiba?
 
Nionavyo mimi, maji ya uvuguvugu yanakua na joto zaidi kuliko hali ya tumbo kwa maana ya ujoto ndo maana ukipiga haya lazima ukashushe vitu vizuri.......Maji ya kawaida yanakua na joto ndogo kuliko hali ya tumbo. Maji ya uvuguvugu hukata kiu zaidi kuliko maji ya kawaida.
 
1: Hiyo hali ya joto kuliko ya tumbo inayosababishwa na maji ya uvuguvugu ina madhara au faida kiafya?
2: Kuna ubaya kama hushushii vitu vizuri baada ya kunywa maji ya moto?
Mwisho kabisa, kwa mtazamo wako, ya uvuguvugu na ya kawaida, yapi yana faida kubwa kitiba?
 
Back
Top Bottom