Kati ya mapacha lazima kuwe na mmoja ana mapungufu.

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Nimekuwa nikisikia kwa watu tofauti kwamba kati ya mapacha lazima kuna moja ana mapungufu(hawawezi wakawa sawa wote),sina uhakika wa hii ila nimesikia tu.
Je kuna ukweli wowote?
 
Upungufu wa nini? Mimi sijaona, ni mmoja Kati ya mapacha. Tumekuwa Na akili, mawazo, hisia vinavyofanana viungo vya mwili vyote sawa, japo tumekuwa Na tofauti kidogo za hapa Na pale. Labda useme ni upungufu gani.
 
Mapungufu ya nini?

Kila mwanadamu awaye yule ana mapungufu yake.
Kwani mapacha si watu kama Mi na wewe tu?
Mapungufu walionao ni kama hii ya kwako ya kurusha thread kama hii ambayo ina mapungufu makubwa.

Pole!
 
Nimekuwa nikisikia kwa watu tofauti kwamba kati ya mapacha lazima kuna moja ana mapungufu(hawawezi wakawa sawa wote),sina uhakika wa hii ila nimesikia tu.
Je kuna ukweli wowote?
Ndiyo!!!!
 
Hakuna mwanadamu aliye kamili.
 
unadanganya watu ,hata mkiwa mapacha haiwezekani mkafanaa akili,mawazo na hisia maana kila mmoja ana moyo wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…