Kati ya Nadir Haroub Cannavaro na Victor Costa nani anapaswa kuwa beki bora wa muda wote Tanzania

junky

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2017
Posts
413
Reaction score
978
Bila ya shaka kila mtu anaufahamu uwezo wa hawa Beki nguli Nadir Haroub cannavaro aliyehudumu timu ya taifa kwa muda mrefu na klabu ya yanga pamoja na Beki machachali Kelvin Yondani Vidic


Nataka nitambue leo yupi anafaa ,anastahiki kuwa beki bora wa muda wote Tanzania kati ya hawa.

1.Nadir Haroub "Cannavaro"
2.Kelvin Yondani "Vidic"
3.Victor Costa "Nyumba"

 
Wa muda wote!? Hakuna hata mmoja kati ya hao aliyekaribia uwezo wa George Masatu au Boniface Pawasa. Labda uzungumzie kwa waliocheza 2005 hadi sasa, lakini si muda wote.
 
Kweli mkuu Kijuram . Costa anawazidi Canavaro na Kelvin lakini kuwa beki bora wa muda wote sidhani .
 
Ila Pawasa na Kelvin naona kama ni aina ya mabeki wenye kufanana uchezaji wao , tofauti yao ni vimo vyao tu . Pawasa anamzidi kidogo urefu Kelvin ila wote ni watu wa kazi haswa . Kutokana na urefu Pawasa alikuwa bora kwa mipira ya kichwa
 
Mkuu tutake radhi wanamichezo kwa kutukosea heshima.

Yaani hao akina Cannavaro ndio wawe mabeki bora wa wakati wote?

Umepata walau kusikia tu habari za akina George Magere Masatu, Jamhuri Kihwelu " Mrema ", Said Mwamba Nassoro Kizota, na wengineo?

Ukija kwa hao akina Yondani, Cannavaro na Victor Costa, ungewashindanisha kwa nafasi ya beki bora kwa miaka 10 au 15 iliyopita walau ingeleta maana mzuri.

Lakini katika hao watatu uliowataja hakuna kama Victor Costa Nampoka Nyumba! Kwangu mimi huyu ndiye Beki bora wa kati kwa miaka 15 iliyopita, alibarikiwa kipaji kikubwa sana na Muumba ikiwemo matumizi makubwa ya akili kushinda hao watumia nguvu Cannavaro na Yondani Mibange.

Niishie hapa!!
 
Kati ya hao watatu, V.C nyumba ni bora, ika kwa habari ya muda wote ngoja wahenga wenye miongo yao ya kutosha hapa Tanganyika waseme...
 
Mi sio shabiki wa Yanga ila nampa credit Cannavaro kwa kudumu kwenye kiwango chake kwa muda mrefu..

Kina Victor costa na wengineo wamekaa kwenye peak muda mfupi
 
Ama kweli simulizi hii naifananisha na ya yule kipofu aliyebahatika kuona kwa muda ! hamad mbele yake kuna punda!!! Laiti kama ungebahatika kumuona George Masatu au Jella Mtagwa au Leodgar Tenga au hata Juma Shabani usingethubutu kuleta kichekesho chako humu!!!!.
 
Uliwahi kumsikia Omari Choggo ( chogochemba), ulimsikia Athumani Juma, Aloo Mwitu. Sibahatishi. Hawa waliwadhibidi vilivyo washambuliaji wa Mehalla el Kubra ya Misri miaka hiyo kwenye nusu fainali ya Mabingwa Afrika. Uliwahi kumsikia Jella Mtagwa, Leodgar Tenga, Isihaka Hassan, Mohamed Bakar Tall, Athumani Juma Chama, George Magele Massatu, Seif Bausi, Godwin Aswile. Orodha ni ndefu labda tuwaorodheshe pamoja kisha tuwapigie kura.
 
Mleta mada . Kevin na Nadir ni mabeki wazuri kwa viwango vyao ila Victor Costa ni habari tofauti kabisa . Huyo alikuwa beki kisiki na fundi haswa . Alikuwa anajiamini na kipaji kikubwa mno .
Kiboko ya wote alikuwa George Masatu, baada yake hajawahi kutokea mwingine. Masatu alikuwa anawageuza washambuliaji wa timu pinzani ndani ya eneo lake la hatari.

Vv
 
Aisee tangu miaka ya 1980 hakuna beki bora kama George Masatu, yaani alikuwa anajiamini na ball control yake ni ya hali ya juu. Jela Mtagwa, Mohammed Tall, Godwin Aswile walijitahidi ila Masatu ni mwisho

Tano bira yangu ya namba 5 naweza kuwapanga hivi:
1. George Magere Masatu
2. Victor Costa Nampoka 'Nyumba'
3. Boniface Pawasa
4. Jella Mtagwa
5. Mohammed Bakari Tall

Huyo Haroub Canavaro kilichomsaidia ni stamina, kuwa mfungaji na kufanikiwa kucheza muda mrefu, vinginevyo namuona kuwa ni mtulizaji na mbutuaji tu.

Vv
 
Hahaha hapo kwenye Mibangee... [emoji23] Ndio wanaonekana Hamnazoo.
 
Kwa kipaji ...uliza mtu yeyote anayejua mpira na kafatilia miaka mingi atakwambia Victor Costa Nyumba alikuwa na uwezo wa pekee mno! Sitowazungumzia akina Masatu sababu hawajatajwa lakini baada ya kizazi cha akina Masatu hakuna beki nchi hii level za Victor Costa. Bahati mbaya hatukumfaidi muda mrefu sababu ya majeruhi (jujuz?) Lakini yule ni habari nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…