Kati ya Nguruwe na ngombe kipi kinalipa?

Kati ya Nguruwe na ngombe kipi kinalipa?

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Kwa waliowahi kufuga nguruwe na ngombe kipi kinalipa?

Kwa mazingira niliyokuwepo ngombe ni biashara sana, yaani maziwa sipati hela ya maendeleo, lita tsh 700 kwa maeneo niliyokuwepo na kupata breed yenye maziwa mengi imekuwa mtihani.

Nakubali ngombe analipa sababu napata samadi ambayo naitumia shambani kwenye parachichi nk na pia ninapouza napata hela nzuri, nguruwe kwangu wanatoa samadi kidogo kiasi kwamba haitoshelezi mashamba.

Bei za nguruwe ni ndogo, ila naiona faida ninapouza watoto wa nguruwe.

Je, huko uliko kipi kinalipa?
 
Vyote hivyo vinalipa kutokana na mazingira uliyopo. Nguruwe Kila siku anatakiwa ale pesa kwa maana ya chakula chake, mazingira unayoishi ndio yataamua bei ya vyakula pia bei itaamuliwa na wapi mradi ulipo.

Japo naamini katika ufugaji wa nguruwe kuliko Ng,ombe kwa sababu uzao wa nguruwe ni WA haraka na pia ukuaji wake ni waharaka. Kumbuka usipeleke njaa zako za pesa kwa nguruwe,,, watengee pesa Yao kabisa sio unawaletea njaa ukahisi utavuna faida
 
Vyote nafuga hata Sasa hivi ,nasema hivi vyote vina pesa Ila ufuge kwa kiwango Cha juu au Cha Kati Kama Ni ngombe uwe na ngombe walau watano wanaokamuliwa sio chini ya Lita 20+

Na nguruwe uwe nao sio chini ya majike 5+dume 1 Ina maana Kila Mara au Kila mwezi utakuwa una vitoto unauza Kama sio kuchinja .
 
Kweli kabisa
 
Nguruwe wana faida, lakini uwe na chakula pamoja na mbegu nzuri. Wanazaa watoto wengi kulinganisha na ng'ome na kwa haraka
 
Back
Top Bottom