kati ya Noah na Harrier kwa familia msaada

kati ya Noah na Harrier kwa familia msaada

Ukwaju

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
13,383
Reaction score
11,197
Mabingwa niamulieni,
kuna gari mbili Noah na Harrier zote nimeahidiwa kuuziwa kila moja kwa 10,000,000/=
Nina familia ya watoto watatu na Mama yao
kwa ajili ya safari za mbali na za mjini km kupeleka watoto shule na mm kazi zangu za kulangua ni gari ipi nzuri kabla sijauuza huu mkweche wangu
Nachanganyikiwa kuhusu gari hizi mbili na zote ni toleo la 1990
  • ipi spea bei ya chini
  • ulaji wa mafuta
  • uhimili wa mikikimikiki
  • ubebaji wa familia km nikiongeza na ka h/g
  • heshima mtaani km mualiko au foleni

nimeweka tu mfano wa hizi picha mwenye mali asingekubali
Harieri cc 2160 wanadai zina VVTi

BF544354_751022.jpg


Noah Liteace cc1990
BF542335_93842d.jpg
 
Du nimeingia Jukwaa silo au nimepotea
au nilitakiwa niwe ndani ya Mada za Magari za mshana jr
RRONDO
hebu saidia japo kidogo nataka kuja huko kununua sasa nasikia ukiweka pesa Benki tena Gari hawakupi na hela anatoa kwenye A/C yake
mshana jr na member wengine badonaomba nishaurini kati ya hizi gari mbili Heriery na Noah TownAce au LiteAce
 
Kwa uelewa wangu wa hizi gari mbili binafsi nakushauri chukua toyota harier hii gari ni nzuri sana na inaheshima mtaani vilevile ni pana kwa hiyo hata upataji wake wa ajali mara nyingi sio sana ukilinganisha na noah,ulaji wa mafuta nahisi hautofautiani sana na noah 12km/L ukiwa hi-way na 8-9km/L ukiwa off high way.
 
Harrier chunguza engine kwanza. Zipo za 6 na za 4. Chukua yenye 2000cc.Ninayo ni nzuri. comfortable. inapambika na ina space ndani.
Noa nimewahi kutumia ila kwa mikoa mingi sasa ni daladala. Hata ununue voxy. Speed ikizidi 100km per hr inahama kwenye njia yaani ni nyepesi.
Ila kama una kijiji ndio saiz yao.
 
chukua NOAH ukapaki airport ule vichwa vya watakaoshuka ATCL mpya (ijayo)
 
Back
Top Bottom