Kati ya Suzuki Escudo na Toyota RAV4 old model gari ipi inafaa katika mazingira magumu?

Kati ya Suzuki Escudo na Toyota RAV4 old model gari ipi inafaa katika mazingira magumu?

parajonse

Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
9
Reaction score
7
Hivi Kati ya Suzuki Escudo na Toyota RAV4 old model kama unaanza maisha,,gari ipi inafaa katika maana ya ulaji wa mafuta, upatikanaji wa spare parts na ustahimilivu wa mazingira

images%20(2).jpg
images%20(1).jpg
 
Escudo ni economic kwenye mafuta, haili mafuta kabisa. Ni gari ambayo nimewaitumia kwa muda mrefu lakini kwa miakaa Kama 8 iliyopita. Nigari ngumu ckuficha, spare zake bei nafuu mtu wa kawaida una muda kabisa.

Sema Sina uwakika kwa Sasa kwenye suala LA spares zake.. Escudo ni gari ya zamani,.sijajua spares Naona haziagizwi Sana siku hizi, nyingi unazoziona ni za zamani.

Ila nikuhakikishiee Kama Wewe ni mkazi WA Dar es Salaam. Spares huwezi kosa zitakuwepo.

Kwa gari ya rava 4 old model ni ngumu Sana, Ila zinakula mafuta sana Labda upate ya diesel naiwe manual transmission
 
Escudo ina sifa unazotaka..tafuta yenye injini code G16(cc1590)...hutojutia

Mkuu upo sahihi kuliko sahihi yenyewe. Gari ya kazi zaidi hapo ni Escudo.

Kwanza ni imara saaana yaani labda aitupe mwenyewe.

Pili mafuta hasa hiyo uliyomtajia yaani waweza jiuliza hii ni gari au bajaji?

Tatu, hii gari ina 4wd najaribiwa kusema ndio inayoongoza. Yaani mnaenda sehemu landcruisers za maana zinakwama hii gari inapita, aiseee sikuamini. Yaani kwenye tope kubwa ni kama inapaa.

Ukiwa ni mtu wa mikoani na njia mbovu mbovu this is the best unit ever ila ina kona ipo mbali balaa...
 
Baadae nitaipiga picha Suzuki Escudo ya mzee wangu no B muione
 
Namba B cha mtoto, ninaifahamu moja namba Tzc ya mwaka 1991, Mara ya mwisho ilisimama mwaka 2010 sio kwa ubovu , Bali jamaa aliichoka , kaiacha imeozea hapo.

Sent
Ziko konki sana kama ni mtunzaji utaichoka mwenyewe, mzee wangu aliinunua 2010 hadi leo iko kama mpya
 
Hizo zote ni gari poa, shida hii suzuki Masawe huwa A/C Yake inasumbua

Ungepata Manual ingekuwa vyema
Yes...nina rafiki yangu ana suzuki short milango mitatu. Kanasumbua sumbua AC...kuna jamaa akachakachua akaweka baadhi ya mifumo ya Toyota kama compressor na kitu kingine sikumbuki ilikuwa nini. Sasa hivi AC yake ni kama upo Antarctica..[emoji210][emoji210][emoji210][emoji210][emoji210][emoji210][emoji210][emoji2415]
 
Gari za Wachaga
Hio Escudo massawe nimemuuzia mtu juzi. Ina engine ya cc1566 kitu kama 1600cc haili wese so ipo njema. Gari hizo ziko nyingi huku Moshi. Wachaga wanazipenda sana maana ndio gari ambazo wengi wamekuwa nazo toka zikiwa kwa wazazi.

Kuhusu spare zipo ila sio zote zinapatikana kirahisi maana ni gari ya kizamani hivyo imeshakuwa phased out sokoni. Watu wanaagiza zaidi ile model mpya yake.
 
Back
Top Bottom