Kati ya Watanzania Milioni 64, Maprofesa ni 226 tu. Baba wa Taifa ndiyo wa kubeba hii aibu

Kwa mujibu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Naibu Waziri wake Mh. Juma Kipanga, Tanzania Ina Maprofesa kamili 63 pekee (full professors). Pia Tanzania Ina Associate Professors 163 nchi nzima.

Hivyo inaonekana Tanzania kuwa profesa sio Jambo la mchezo. Pia ukigawanya kwa kozi zilizopo Tanzania, utakuta kila kozi Ina full profesaa watatu Kama sio wawili. Hivyo, tujitahidi kusoma ili kuziba pengo la hao Maprofesa wakistaafu.
 
Na maprofessa 41 ni wahaya tu, sasa ukiondoa wahaya wakirudi kwao uganda Tanzania itabakiza maprofessor wangapi?
 
 
Kwa elimu hii ya TANZANIA..mbona hao wengi sanaaa ..... Walaitakowa wa5 au 6 tu ....
 
Wakati mnakandya msisahau MUHAS ni top university kuliko hizo za Kenya
 
wanastaafu sasa hao maprofesa,,hawataki hata !!!!
wana felisha MADOKTA ili kuendelea kulinda nafasi zao
 
Huku Kijijini kwetu Kuna jamaa hajasoma anafuso tatu zinatusaidia kwenda mjini.sisi tunamuona Kama ni zaidi ya profesa.
Acheni kujifariji na wajasiariamali. Kuwa Professor kwa Tanzania sio mchezo ndio maana wapo 63 pekee
 
Hata wangekuwa 3,000.000 wana msaada au umuhimu gani? Akina Mkumbo wamerubuniwa, wengine wanauza bandari, wameacha kujikita kwenye majukumu yao ya kitaaluma wamekimbilia siasa wanauza nchi
Ujinga wa baadhi ya Maprofesa hauufanyi uprofesoor kuwa mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…